EU YAKARIBISHA MAKUBALIANO YA AMANI YA SERIKALI YA KONGO DR NA WAPINZANI

Umoja wa Ulaya umekaribisha makubaliano ya amani baina ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wapinzani wa nchi hiyo.
Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya, na Neven Mimica, Kamishna wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa na Maendeleo cha umoja huo, sanjari na kukaribisha kutiwa saini makubaliano hayo ya kisiasa baina ya pande mbili nchini Kongo DR, wameonyesha pia matumaini kwamba mapatano hayo yatapelekea kupatikana amani na usalama wa kudumu nchini.
Jean-Marc Ayrault, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa
Naye Jean-Marc Ayrault, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amesema, makubaliano kati ya serikali ya Kinshasa na wapinzani ni mwanzo wa kuikwamua nchi hiyo kutokana na mgogoro wa kisiasa. Serikali na wapinzani wa nchi hiyo walifikia makubaliano hayo chini ya uangalizi wa maaskofu wa Kanisa Katoliki.
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Rais Joseph Kabila ataendelea kuwa rais hadi mwishoni mwa mwaka huu. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, utawala wa rais huyo ulifikia tamati tarehe 19 mwezi Disemba uliopita.

0 comments: