NALAANI VITENDO HIVI VYA KINYAMA VYA KUPIGANA WENYEWE KWA WENYEWE
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:00 PM
Ndugu
Augustino Mtitu mkulima wa kitongoji cha Upangwani, Kijiji cha Dodoma
Isanga, Kata Ya Masanze Jimbo la Mikumi aliyechomwa Mkuki na wafugaji wa
kwanza kushoto.
Kwanza
niruhusu nikupe Pole ndugu yangu kwa lililokukuta. La msingi Serikali
inatakiwa kujua, tunaposema maoni yetu pale Bungeni tunamaanisha. yako
mambo unaweza yafanyia utani lakini hapa tulipofika si kwa kuchukulia
mzahamzaha.
Waziri
muhusika haya hauyaoni au niliposimulia juu ya Wananchi wa Jimbo la
Chalinze kupigwa , kuvunjwa migongo na mwengine kupigwa mshale wa goti
na kumpa ulemavu wa maisha mlidhani natania. Sasa hili liwe fundisho.
Serikali ni lazima ije na majibu sahihi juu ya kunusuru vita ya wenyewe
kwa wenyewe .
Jana mtu
kavunjwa mgongo, mwengine mlemavu leo kapigwa mkuki wa mdomo umetokea
shingoni. Lini tutasikia kilio hiki? Serikali sikieni kabla Damu ya
watanzania wanyonge wanaotegemea kilimo kama kiinua mgongo chao
hawajapotea. Kuna sheria, na mipango ya matumizi bora ya Ardhi. Nini
kinafichwa?
Binafsi
Nalaani Vitendo hivi na kuiasa Serikali yangu kujipanga vizuri kabla
mambo hayajaharibika. yalianza Kilosa, Mvomelo, Chalinze, Handeni,Kiteto
na sasa Mikumi ( kutaja maeneo machache) .Serikali jipangeni, kabla
hapajachafuka.
RIDHIWANI KIKWETE, MBUNGE WA JIMBO LA CHALINZE.(P.T)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: