BIDHAA YA NAFAKA SOKO LA MWANGA ,,, YAPANDA BEI KIGOMA


NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

 WAFANYABIASHARA wa Bidhaa ya Mahindi,Unga na Mchele Soko la Mwanga Manispaa ya Kigoma Mjini Mkoa wa Kigoma  inazidi kupanda bei mwezi hadi mwezi mkoani Kigoma, hali inayochangiwa na ukosefu wa ghala la Chakula sanajari na uboreshaji wa miundombinu ya  barabara  hasa  Kigoma -Mpanda  iwekewe lami ili kuondoa gharama za  kupanda kwa bidhaa hizo.
Akizungumza na mwandishi wetu,  mmiliki wa mashine za kusaga  nafaka  Jiti Rubibi alisema mwanzoni mwa mwezi Septemba debe moja la mahindi ni sh.11,000   sawa na sh.66 kwa gunia moja kwa mahindi yanayotoka  wilayani kasulu na uvinza lakini mwanzoni mwa mwezi huu debe moja  kwa bei ya jumla hulangua kwa  sh.13 sawa na sh.78 kwa gunia moja .
Alisema sababu kubwa ni kukosekana kwa ghala la chakula mkoani humo, ambapo serikali ingedhibiti uzwaji wa nafaka hizo na kipindi hiki cha kuadimika kwa nafaka hizo ghala ingepunguza ukali wa bei ya bidhaa hiyo sambamba na kuboreshwa kwa barabara ya kigoma kwenda mpanda ambako wafanyabishara huagiza katika ghala la chakula mkoani humo.
Kwa upande wa muuza mahindi Matilda Salehe na muuza unga Khadija Lucas kwa nyakatio tofauti wakiri mahindi kupanda bei kwa kuwa awali walikuwa wakinunua gunia kwa sh.65 na debe wakilangua kwa sh.12,000 kwa kipindi cha mwezi uliopita,lakini sasa wanalangua debe moja kwa sh.78,000 mahindi ya kutoka mpanda.
Khadija alisema kutokana na hilo huwauzia wateja wanaofika katika mashine za kusaga nafaka kilo moja kwa sh.1,000  na wanaokwenda kuuza maduka ya mitaani huwauzia wateja kilo moja kwa sh.1200 na wengine 1100 kulingana na gharama za usafiri wa kufikisha eneo husika na kuiomba serikali iboreshe miundombinu ya barabara ili kupunguza gharama za uingizaji wa nafaka hizo.
                                                                                          
Naye muuzaji wa bidhaa ya mchele Soko la Mwanga Manispaa ya kigoma Ujiji Fedirick Emanuel alisema awali walikuwa wakiuza kilo moja ya mchele kwa sh.1000 hadi sh.1,200  na gunia moja walikuwa wakilangua mkwa sh.120,000 lakini kuanzia mwanzoni mwa mwezi huu gunia moja la mchele wanalangua kwa sh.130,000 ambapo huwauzia wateja kilo moja kwa sh.1400 hadi 1500 kwa mchele msafi.
Emanuel alisema kwa mchele unaolimwa mkoani kigoma  kata ya kalya wilaya ya Uvinza wakulima wanapeleka bidhaa hiyo nchini DRC-Congo na hulazimika kulangua mkoani mpanda hali  mbaya ya barabara inachangia  kuongezeka kwa  gharama za usafirishaji hivyo  hawana budi kufidia hilo kwa mlaji.
Mwisho.

0 comments: