WAZIRI JENISTA MHAGAMA AKUTANA NA KAMATI YA URATIBU WA MAAFA MKOA WA KAGERA

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)  Jenista Mhagama (Mb) akifungua kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera Septemba 18, 2016, kulia kwake ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua
 Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama, wakati wa mkutano wao uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Salum Kijuu akiwasilisha taarifa ya tathimini ya hali ya waathiri wa Maafa ya Tetemeko la Ardhi mkoani hapo wakati wa kikao cha Kamati ya Mkoa ya Uratibu wa Maafa.
 Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro akichangia hoja wakati wa Kikao cha Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu Mkoa Kagera
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Uratibu wa Maafa Mkoa wa Kagera wakiendelea na kikao cha kujadili na kufanya tathimini ya hali ya athari ya Maafa ya Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera. Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu

0 comments: