WATU 17 WAPOTEZA MAISHA WAKATI WA MAANDAMANO YA UPINZANI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:34 AM
Katika
mtaa wa Limete, mjini Kinshasa, mamia ya watu walikusanyika katika eneo
linalojulikana kwa jina la Lumumba, DRC, Jumatatu Septemba 19, 2016.
Wizara ya
mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba
watu 17 ndio wamepoteza maisha katika maandamano ya upinzani wakidai
kuondoka madarakani kwa rais Joseph Kabila atakapomaliza muhula wake
mwezi Desemba mwaka huu.
Waziri wa
Mambo ya Ndani wa DR Congo, Evariste Boshab aamesema watu 17 wamepoteza
maisha katika maandamano hayo, ikiwa ni pamoja na askari polisi watatu.
Watu hawa
wamepoteza maisha wakati wa maandamano yaliyofanyika Jumatatu hii
katika mji wa Kinshasa na miji mingine ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo.
Kwa
mujibu wa msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congoongo,
Lambert Mende, askari polisi walichomwa moto wakiwa hai na raia
waliouwawa walikuwa miongoni mwa waandamanaji.
Watu kadhaa wamekamatwa. Miongoni mwao ni wabunge wawili wa upinzani, ikiwa ni pamoja na Martin Fayulu.
Upinzani
nchini DR Congo ulifanya maandamano katika miji kadhaa nchini kote
Jumatatu hii, wakidai uchaguzi wa urais ufanyike mwezi Novemba, kama
inavyotakiwa na Katiba.
Lakini
uchaguzi wa urais hauwezi kufanyika kabla ya mwisho wa mwaka, kulingana
na viongozi wa vyama vinavyounga mkono serikali na viongozi wa Tume ya
uchaguzi ya Taifa. RFI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: