MADEREVA WA MALORI KUTOKA TANZANIA NA KENYA WAOKOLEWA DRC


Madereva nane wa malori kutoka nchini Tanzania na wengine wanne kutoka Kenya wameokolewa baada ya kushikwa mateka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Madereva hao walitekwa nyara katika mkoa ulio kusini wa Kivu siku ya Jumatano.

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Tanzania ilisema kuwa watekaji nyara wao walikuwa wakiitisha fidia ya dola 4,000 kwa kila dereva.
Hata hivyo waziri wa masuala ya ndani nchini Congo Zakwani Salehe, alisema kuwa hakuna fidia iliyolipwa na ni wanajeshi waliowaokoa madereva hao.

Aliwataja watekaji hao kama majambazi na haijabainika ikiwa walikuwa na uhusiano na kundi lolote la waasi linaloendesha shughuli zake mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Bukavu anasema kuwa visa vya utekaji nyara kwa fidia vinazidi kuongezeka.

0 comments: