KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YAANZISHA HUDUMA YA WHATSAPP BURE KWA WATEJA WAKE
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:07 AM
Meneja
Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez akizungumza na
waandishi wa habari na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa huduma
hiyo uliofanyika Hoteli ya Hyatt Regence Kilimanjaro Dar es Salaam jana.
Wadau mbalimbali na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Hapa kila mgeni mualikwa akiwa busy na simu yake kwenye uzinduzi huo.
Ni kama wanasema 'tumependeza sana ngoja tujipige picha'.
Wanahabari wakifurahia jambo kwenye uzinduzi huo.
Hapa ni furaha tupu kwa wanahabari.
Washereheshaji katika uzinduzi huo, Taji Lihundi na mwenzake wakifanya vitu vyao.
Burudani ikiendelea.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na viongozi wenzake katika uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Diego Gutierrez (katikati), akiwa na washereheshaji wa uzinduzi huo.
Makofi yakipigwa kufurahia uzinduzi huo.
Wanahabari mabloggers wakiwa katika picha ya pamoja na msanii Lucas Muhuvile 'Joti'.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya Tigo, imetangaza huduma ya bure ya WhatsAap kwa watumiaji wa huduma hiyo.
Akizungumza
Dar es Salaam jana katika uzinduzi huo,Meneja Mkuu wa Tigo Diego
Gutierrez amesema kuwa wateja waote wa tigo wanaotumia vifurushi vya
intaneti vya kampuni hiyo kwa wiki na mwezi watapata huduma ya whatsaap
bure.
Alisema
kuwa ni mara ya kwanza kwa kampuni ya simu kitoa ofa ya bure ya
mtandao huo wa jamii nchini pia kampuni ya tigo ina wateja zaidi ya
milioni 10.
"Unajua
huduma ya whatsaap ambayo ni maarufu kwenye kutumia ujumbe kwa njia ya
simu inawatumiaji zaidi ya milioni nane nchini tanzania na duniani
inatumiwa na watu wapatao milioni 900,pia huduma hiyo inasaidia
watumiaji kubadilishana habari ,ujumbe,video na miito ya sauti"alisema
Gutierrez
Alisema
kuwa kuanzia sasa na kuendelea kwa wateja wote wa tigo wanaonunua
vifurushi vyetu vya wiki au mwezi watakuwa na fursa ya kufurahia
whatsaap bure.
Aliongeza
kuwa huduma ni kwa watumiaji wa smartphone na kupata huduma bure ya
whatsaap kwa wateja tigo imejikita katika kuboresha mabadiliko kwenye
maisha ya kidigitali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: