UKIWATENDEA WEMA WAZAZI UTAPATA RADHI


Katika enzi za Nabii Mussa ‘alayhi salaam, Ilitokezea
siku ambayo Nabii Mussa ‘alayhi salaam, alimuuliza
ALLAH subhanahu wata’ala: “EWE ALLAH, NANI ATAKUWA
RAFIKI YANGU PEPONI?” ALLAH AKAMJIBU: “MUUZA
NYAMA.” Akashangaa sana Nabii Mussa ‘alayhi salaam
akijiuliza, kwanini muuza nyama awe ni rafiki yangu
peponi? Hivo akamuuliza Allah, ni wapi nitampata
huyu mtu? ALLAH akampa maelekezo ya alipo huyo
kijana. Akafuata maelekezo hayo Nabii Mussa ‘alayhi
salaam mpaka akafika na kumkuta huyo kijana
akikata nyama, kisha akachukua kiasi cha nyama
nakuondoka nacho akielekea nyumbani. Basi Nabii Mussa
‘alayhi salaam akawa anamfuata huyu kijana mpaka wakafika nyumbani kwake, akamuuliza: “Jee, hutojaalia msafiri kuwa
mgeni wako?” Yule kijana akajibu “Na kwanini isiwe
hivyo? Basi, karibu ndani.” Hapo Nabii Mussa akawa anatizama vitendo vya yule kijana, tangu akiosha nyama, kuikata,
kuipika hadi kuipakua katika sahani. Kisha, akateremsha kikapu kikubwa na ndani yake alikuwemo bibi ‘ajuza, akamueka
kwenye mikono yake, kama mzazi anavyomueka mwanawe,
kisha akampangusa na kuanzakumlisha nyama aliopika kabla kwa mikono yake huku akimchagulia uzuri, kisha akawa anampangusa kwa kitambaa, na baada ya kumaliza akamrejesha kwenye kile kikapu. Nabii Mussa ‘alayhi salaam alikuwa akiangalia haya
yote na aligundua kuwa kila anapomlisha tonge yule bibi,basi akinong’ona maneno Fulani. Hivyo, Nabii Mussa akamuuliza yule kijana: “huyu ni nani kwako?” Akajibu: “Ni Mama yangu. ikujaaliwa na uwezo wakutafuta chakula na kumpikia mama yangu akala
uzuri, hivyo ninapomaliza kazi yangu kwa siku, huchukua kile katika kilichobaki na humpikia nikamlisha kwa vile yeye ni mtu mzima sana na sina uwezo wakuajiri mfanayakazi akanisaidia
kumshughulikia.” Nabii Mussa ‘alayhi salaam akaendelea umuuliza: “Sawa. Ila ni nini huwa anasema kila
unapomlisha tonge?” Akajibu kijana: “Huniombea dua, Ewe Mola, mjaalie mwanangu awe ni rafiki wa Mussa peponi! ” Subhanallah! Angalia umuhimu wa dua ya mama! Ni dua ya mama yake
alioikubali Allahsubhanahu wata’ala! Mtume swalla llahu ‘alayhi
wasallam anasema: “Pepo ipo chini ya nyayo za Kimama ” (Ahmad, Nasai). SURAT AL AN'KABUT,8: NA TUMEMUUSIA MWANAADAMU KUWAFANYIA WEMA WAZAZI WAKE. ALLAH atujalie tuwe katika watu watakaofanyia wema wazazi wao na kupata pepo ya ALLAH kwa rehma zake. Aaamin.

0 comments: