Kamanda
Mtoi alifariki dunia baada ya kupata ajali, Jumamosi ya Septemba 12,
mwaka huu, eneo la Magamba alipokuwa njiani kurejea nyumbani kwao Mkuzi
baada ya shughuli za kampeni jimboni humo.Ofisi
ya Katibu Mkuu na Chama kwa ujumla kimempoteza mmoja wa wanachama,
mtendaji na kiongozi mahiri kabisa katika wakati ambapo mchango wake
ulikuwa ukihitajika sana.
Mazishi
ya Ndugu Mohamed yamepangwa kufanyika Leo saa 7 mchana nyumbani kwao
Mkuzi, Lushoto ambapo Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mheshimiwa Freeman
Mbowe atashiriki.
Chama kwa kushirikiana na familia kinafanya uratibu wa msiba huo na taarifa zaidi zitaendelewa kutolewa.Pamoja
na mambo mengi, Ndugu Mohamed atakumbukwa sana kwa namna alivyoratibu
na kusimamia uendeshaji wa Kanda za Chama kupitia idara yake chini ya
Kurugenzi ya Oganaizesheni, Mafunzo na Uratibu wa Kanda.Kama
inavyojulikana, dhana ya kuendesha chama kupitia Kanda, imekuwa ni
utekelezaji kwa vitendo wa mojawapo ya sera muhimu za chama, iitwayo
Mfumo Mpya wa Utawala, hivyo Ndugu Mohamed alikuwa aliaminika na kupewa
majukumu makubwa ya kuhakikisha chama kinathibitisha kwa Watanzania kuwa
mawazo mbadala ya mabadiliko yanawezekana kwa manufaa ya taifa letu.Wasomaji
wa kupitia njia mbalimbali za mitandao ya kijamii na baadhi ya
magazeti, watakumbuka namna Mohamed alivyokuwa na mchango mkubwa katika
kupigania chama kutokana na imani yake kubwa katika kupigania mabadiliko
na kutoyumba.
Chama
kinatoa pole kwa familia ya Ndugu Mohamed kwa kumpoteza baba, mmoja wa
nguzo muhimu na mtu wa karibu katika maisha yao. Tunaomba Mwenyezi Mungu
awafanyie wepesi na kuwapatia moyo wa ujasiri katika wakati huu mgumu.
Aidha
chama kinatoa salaam za pole kwa ndugu, jamaa, marafiki wa Mohamed
halikadhalika viongozi, wanachama, wapenzi, mashabiki wa CHADEMA na
Watanzania wote walioguswa na msiba huo.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
Imetolewa leo Jumapili, Septemba 13 na;
Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: