BREAKING NEWZZ...RAIS PAUL KAGAME WA RWANDA APATA AJALI KENYA.

Watu wawili wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha mojawapo ya magari ya msafara wa magari ya Rais Paul Kagame nchini Kenya.
Rais Mwenyewe hata hivyo hakujeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi katika eneo la Limuru eneo la Kati mwa Kenya.

Gari hilo hata hivyo lilipoteza mwelekeo likiwa mbali na msafara wenyewe.Dereva wa gari hilo alipoteza mwelekeo katika barabara kuu ya Nairobi-Limuru.

Waliojeruhiwa walipelekwa hospitalini.

Rais Kagame alikuwa anarejea mjini Nairobi kutoka katika kongamano la magavana wa Kenya mjini Naivasha katika bonde la ufa .

Kwa sasa Kagame anakutana na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Rais.

Kagame alialikwa kuhudhuria kongamano la Magavana nchini Kenya kuhusu uongozi mzuri na utawala bora.

Aliwahutubia Magavana hao siku ya Jumatatu na kuwashauri kuwahusisha wananchi katika maamuzi yao ya maendeleo

0 comments: