KENYA NA UGANDA KUZINDUA KITUO CHA PAMOJA MPAKANI BUSIA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:33 PM
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Uganda
Yoweri Museveni wanajumuika pamoja leo Jumamosi kwa hafla maalum ya
uzinduzi rasmi wa kituo cha pamoja cha kutoa huduma za mpakani baina ya
Kenya na Uganda, mjini Busia.
Uzinduzi wa kituo hicho ni mojawapo ya hatua za kurahisisha biashara
na uhamiaji miongoni mwa raia wa nchi zote mbili, chini ya mchakato wa
kutekeleza itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashiriki. Vituo vingine kama
hivyo vimejengwa kwenye mipaka ya nchi hizo na Tanzania pamoja na
Rwanda.
Marais Uhuru Kenyatta na Yoweri Museveni watakariri
umuhimu wa kuondoa urasimu ili kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii
kufanyika kwa utaratibu tena kwa ufanisi zaidi.
Uzinduzi wa soko la pamoja la Afrika Mashariki
Florence
Atieno ambaye ni mwenyekiti wa kundi la wanawake wafanyabiashara wadogo
wadogo wa eneo la mpakani la Busiaanasema kabla ya kupata huduma hiyo
mpya wafanya biashara walikuwa wanakabiliwa na changa moto chungu nzima.
''Hapo
awali sisi kama wafanya biashara wa mpakani tulikumbana na changa moto
si haba. Wengi walikuwa wanatumia njia za mkato na hivyo kupatana na
masaibu chungu nzima kama vile wanawake kubakwa, kupoteza mizigo na hata
watoto. Lakini kwa sasa, mambo yamebadilika. Kutokana na kituo hiki cha
pamoja, gharama ya kufanyia biashara imepungua na tunapata faida. Pia
usalama wetu umeimarika''. Amesema Florence Atieno.
Busia ni
kivukio muhimu kwa wafanya biashara wa mataifa ya kanda ya Afrika
Mashariki. Mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha pamoja kimefadhiliwa kwa
kima cha zaidi ya dola milioni 12 kupitia shirika la mpango wa maendeleo
la Uingereza, DFID, kwa ushirikiano na serikali ya Canada.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: