KANUNI ZA MAADILI YA TAALUMA YA MAWASILIANO KWA UMMA KUANDALIWA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:34 AM
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicolaus William (kushoto)
na Rais wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) Bw.Loth Makuza (kulia) wakionyesha Katiba ya
chama hicho kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa umma waliyohudhuria uzinduzi wa
chama hicho (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.
NA
ANITHA JONAS – WHUSM
Idara
ya Habari Maelezo pamoja na Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST)
wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuandaa
Kanuni za Maadili ya Taaluma ya Mawasiliano kwa Umma kwa kuzingatia maslai ya
taifa.
Kauli
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William alipokuwa akizindua chama
cha PRST chenye lengo la kuongeza ueledi kwa wanataaluma ya mawasiliano kwa
umma nchini .
“Ningependa
kuona chama hichi kinakuwa mstari wa mbele katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa
wanataaluma wake kama lilivyolengo kuwa chama kitajikita zaidi katika kuongeza
weledi kwa wanatansia pamoja na kuleta mabadiliko ya kiutendaji katika sekta ya
mawasiliano nchini kwa kulingana na mahitaji ya soko,”Bw.William.
Akiendelea
kuzungumza katika uzinduzi huo Naibu Katibu Mkuu huyo alisisitiza kuwa ni vyema
wadau wote wa taaluma ya mawasiliano kwa umma watambue umuhimu wa chama hichi
kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kukikuza,kukiendeleza na kukijengea misingi
imara itakayodumu na kuleta tija ndani ya taifa.
Kwa
upande wa Mwakilishi wa Msemaji Mkuu wa Serikali kutoka Idara ya Habari Maelezo
Bw.Jonas Kamaleki alieleza kuwa serikali inaunga mkono jitihada za kuanzishwa
kwa PRST na iko tayari kutoa ushirikiano wakati wote.
“Serikali
ingependa chama hichi kuwa na mikakati madhubuti na utekelezaji wenye tija na hata kuwa mfano kwa Afrika
Mashariki bila ya kujali kuchelewa kwa kuanzishwa kwake,”Bw.Kamaleki.
Naye
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Shule ya Habari na Mawasiliano kwa Umma
Dkt.Dietrick Kaijanangoma alitoa nasaha kwa Maafisa Uhusiano wa taasisi
mbalimbali nchini ya kuwataka kuwa wabunifu na kufanya tafiti ndogo na kubwa
kwa ajili ya kuimarisha taasisi zao na zaidi kujifunza kwenda na wakati kwa
kutambua mahitaji ya umma.
Pamoja
na hayo nae Rais PRST Bw.Loth Makuza alitoa shukrani kwa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania Awamu ya Tatu Mhe.Benjamin
William Mkapa kwa kuanzisha sekta ya habari nchini
Halikadhalika
Bw.Makuza alitoa ombi kwa taasisi mbalimbali kuunga mkono uanzishwaji wa chama
hicho pamoja na wanataaluma kujitokeza
kwa wingi na kujiunga na chama utaratibu wa kujiunga unapatikana kupitia tovuti
ya www.prst.or.tz.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William
(watatu kushoto) akikata utepe wa Katiba ya Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania
(PRST) kuashiria kuzinduliwa kwa chama hicho leo jijini Dar es Salaam,aliyeshika
Katiba hiyo (kulia) ni Rais wa PRST Bw.Loth Makuza.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Nicolaus William(wanne kushoto)akimkabidhi cheti Bw.Innocent Mungy kilichotolewa na uongozi wa chama Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) kwa kutambua mchago wake katika kuanzishwa kwa chama hicho mara baada ya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya viongozi wa Chama cha Uhusiano wa Umma Tanzania (PRST) wakiwa katika picha
ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Bw.Nicolaus William(aliyeketi wanne kushoto) mara baada ya uzinduzi wa chama
hicho leo jijini Dar es Salaam na watatu
kutoka kulia) ni Rais wa PRST Bw. Loth Makuza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: