Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini
Dar es Salaam Mei 11, 2017
|
RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA AWASILI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFIULI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:38 AM
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akikagua Gwaride la Heshima aliloandaliwa na Jeshi la
Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akipunga mkono wakati akiwasili Ikulu akiwa pamoja na
mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na mgeni wake
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza mazungumzo yao Rasmi Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akipiga ngoma wakati alipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara
baada ya kumaliza mazungumzo na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma,
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma kabla ya kuanza kuzungumza na wanahabari Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akisoma hotuba yake wakati akizungumza na wanahabari Ikulu
jijini Dar es Salaam.
NA BEATRICE LYIMO NA IMMACULATE MAKILIKA- MAELEZO
SERIKALI za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Afrika ya Kusini zasaini mikataba mitatu ya ushirikiano katika sekta mbalimbali
zitakazosaidia kukuza uchumi wa nchi hizo mbili.
Hati za mikataba hiyo zimesainiwa leo Ikulu
Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa Marais wawili Dkt. John
Magufuli na Jacob Zuma na waandishi wa habari.
Mikataba iliyosainiwa baina ya nchi hizo mbili
ni hati ya muhtasari wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya
Marais kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini
uliolenga kuboresha makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mkutano huo.
Hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya
Bi Anuwai kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini, inayolenga kuboresha
ushirikiano katika sekta ya wanyamapori na uhifadhi.
Huku hati nyingine ikiwa ni makubaliano ya ushirikiano
katika sekta ya uchukuzi kati ya Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini
uliolenga kuboresha ushirikiano katika sekta ya uchukuzi.
Akizungumza wakati wa mkutano huo Rais Magufuli
alisema ziara ya Rais Zuma imekwenda sambamba na mkutano wa kwanza wa tume ya
Marais ambapo ulibainisha baadhi ya maeneo ya makubaliano.
Rais Magufuli alisema kuwa maeneo ya makubaliano hayo
yalilenga kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya
nchi hizi mbili na njia za kundoa vikwazo vinavyokwamisha biashara baina yao.
“Hali ya biashara ya Afrika Kusini nchini kwa mwaka
2016 ni takribani Tsh Trilion 2.4 na uwekezaji wake ni Dola za Kimarekani
803.15 milioni iliyopelekea kupatikana kwa ajira kwa watanzania 20,916”alisema
Rais Magufuli
Rais Magufuli alitaja maeneo mengine ya makubaliano
kuwa ni kushirikiana katika sekta ya viwanda ambapo amewakaribisha
wafanyabiashara kutoka nchini Afrika Kusini ili kuwekeza katika kujenga
viwanda vya kusindika mazao na hivyo kukuza uchumi.
Kwa upande wa Sekta ya miundombinu na nishati
wamelenga katika kuimarisha reli ya kati na upatikanaji wa umeme, ambapo
Rais
Dkt.Magufuli amemwomba Rais Zuma kutumia ushawishi wake katika Umoja wa nchi
zenye uchumi unaokua kwa kasi (BRICS) ili kuisaidia Tanzania kupata mkopo kwa
gharama nafuu, kwa lengo la kuendeleza ujenzi wa miradi ya reli ya kati na
umeme.
Vilevile, Marais hao wamekubaliana kubadilishana
uzoefu na wataalamu kupitia sekta ya utalii ikiwemo kuwakiribisha wawekezaji
kutoka nchi ya Afrika Kusini kuwekeza kwa kujenga hoteli za kitalii
pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.
Maeneo mengine ya makubaliano ni pamoja na sekta
za madini kwa kubadilishana uzoefu na utaalamu, afya kwa kuwakaribisha
wawekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kutengeneza dawa, elimu, sayansi na
teknolojia ambapo Rais Zuma amekubali kupokea wataalamu wa lugha ya kiswahili
watakaofundisha Afrika Kusini.
Rais Zuma alisema wataendelea kuimarisha uhusiano
uliopo baina ya nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na kukuza umoja wa Afrika ili
kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyokabili bara hilo.
“Tumefurahi kusaini mikataba hiyo leo, pamoja na
kupata taarifa ya mawaziri iliyojitosheleza katika kuainisha maeneo ya
ushirikiano na utekelezaji wake itakayosaidia kuleta maendeleo katika nchi hizi
mbili” alisema Rais Zuma
Rais Jacob Zuma anakamilisha ziara yake ya siku mbili
leo usiku iliyolenga katika kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya
nchi hizi mbili, ikiwa ni pamoja na kuanisha maeneo mapya ya ushirikiano
yatakayochochea maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Rais wa Afrika
Kusini Jacob Zuma akizungumza jambo na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara
baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Rais Dkt. John Pombe Magufuli
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais
wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kufika ofisini kwake Ikulu jijini Dar
es Salaam.
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akifurahia jambo pamoja na Mama Sizakele Zuma Mke wa Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma aliyeambatana na msaidizi wake Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Vikundi vya
Matarumbeta vikitoa burudani wakati Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam. (PICHA NA IKULU)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: