Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni
akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza la Wanawake wilayani
Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa
kushirikiana na wafungwa.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,
mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,
akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa
lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na
wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi
huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
Mbunge wa
Jimbo la Mpwapwa, Mheshimiwa George Lubeleje , akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na
wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza
hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika
wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa, akizungumza
wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa
na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na
wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi
huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa
pili kulia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dk.
Juma Malewa (kulia) kuelekea katika eneo lilipo Gereza la Wanawake
Mpwapwa, lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa
kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi
milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Wananchi
wa Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa
Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni
askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu
jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya
Mpwapwa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu, MOHA
Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya
Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana
na changamoto za makazi ya askari wa jeshi hilo hapanchini.
Akizungumzia
changamoto za Makazi ya askari wa Jeshi la Magereza Nchini, wakati wa
uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema
Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari
iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.
“Nawaomba
askari wetu nchi nzima wawe na subira Serikali inatambua na
inashughulikia changamoto ya makazi ya askari na tayari tuko katika
mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa
nyumba takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na
familia zao,” alisema Masauni.
Awali
akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la
Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa
na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa kushirikiana na wafungwa
kama sehemu ya utekelezaji wa amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya
kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo,ujenzi
na ufundi mbalimbali.
Ujenzi wa
Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia
kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika
Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa ndugu wa
wafungwa kusafiri mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: