MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI YALIYOFANYIKA JANA MEI 3, 2017 MEI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akipitia ratiba ya hafla ya Kongomano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani Mei 3, 2017 yaliofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar. 
Mc wa Kongamano la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani Ndg Suleiman Seif akitowa maelezo la kongamano hilo la kuadhimisha lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.  
Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chande Omar akitowa maelezo wakati wa maadhimishi ya Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani ilioadhimishwa Zanzibar katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mukajanga akitowa maelezo wakati wa Kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar. 
Wageni waalikwa na Viongogozi wa Vyombo vya habari Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo. 
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Habari Tanzania Hassan Abdallah Mitawi akitowa maelezo ya hafla hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja kutowa machache na kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuhutubia Kongamano hilo la kuadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud akitowa nasaha zake wakati wa kongamano hilo kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuhutubia hadhara hiyo ya waandishi wa habari mbalimbali walioko Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akihutubiwa wakati wa Kongamano la Kuadhimisha Siku ya Vyombo vya Habari Duniani huadhimishwa kila mwaka mwezi wa mei 3, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Zanzibar.



Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar Ndg Chane Omar akiwasilisha Mada ya kuhusu Umakini wa Fikra kwa wakati muhimu Nafasi ya Vyombo vha Habari katika Kuimarisha jamii zenye Amani, Haki na Ujumuishwaji, wakati wa kongamano hilo la Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar
MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Ndg Ali Uki akitowa Mada kuhusiana Uchambuzi wa Sheria za Habari Zanzibar wakati wa Kongamano hilo.



MWANDISHI wa Habari Muandamizi Ndg Enzi Talib akichangia mada zilizowakilishwa wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani lililofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Kilimani Zanzibar

Makamu wa Pili wa rais wa zanzibar balozi seif ali iddi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyombo vya habari Zanzibar. 
imetayarishwa na othmanmapara.

0 comments: