Kufuatia kuvuja barua ya siri ambayo Mfalme
Salman wa Saudi Arabia ameiandikia Wizara ya Fedha ya nchi hiyo,
imebainika kuwa utawala huo wa kifalme utatumia dola milioni 68 kwa
ajili ya kugharamia mapokezi ya Rais Donald Trump wa Marekani
anayetazamiwa kuitembelea nchi hiyo mwishoni mwa mwezi huu.
Sambamba na kukaribia safari ya Trump nchini Saudia, waraka wa
siri unaotoka Baraza la Ufalme wa nchi hiyo na unaosisitiza kuchukuliwa
hatua za haraka umesambazwa katika mitandao ya kijamii ukionyesha
gharama za fedha zitakazotumika kwa ajili ya kumlaki rais huyo wa
Marekani.
Kwa mujibu wa waraka huo, ofisi ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Aal
Saud imeiandikia barua Wizara ya Fedha kuitaka ifanye maandalizi
yanayohitajika kwa ajili ya kumlaki rais wa Marekani na pia kuitaka
iafiki kuidhinisha bajeti ya mapokezi ya dola milioni 68 kwa ajili
kugharamia kikao cha pamoja baina ya Waarabu na Marekani.
Trump anatazamiwa kufanya safari nchini Saudi Arabia mwishoni mwa
mwezi huu wa Mei. Duru za kuamimika zimeripoti kuwa lengo kuu la safari
hiyo ya rais wa Marekani ni kufunga mikataba ya kuiuzia Saudia silaha
zenye thamani ya makumi ya mabilioni ya dola.
Hii ni katika hali ambayo kutokana na kushuka bei ya mafuta, gharama
za vita dhidi ya Yemen na kuyasaidia kifedha makundi ya kigaidi katika
eneo uchumi wa Saudia umezorota ambapo idadi ya watu wasio na ajira
nchini humo imefika watu milioni 27 ikiwa ni zaidi ya asilimia 11.
Aidha kutokana na kuanzisha vita dhidi ya Yemen na kukoleza moto wa
vita katika nchi nyengine za eneo la Mashariki ya Kati, Saudi Arabia ni
nchi ya tatu inayonunua silaha kwa wingi duniani huku asilimia 99 ya
silaha za nchi hiyo ikiwa inaagizwa kutoka nje.../
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: