BRIGEDIA JENERALI DEHQAN: SAUDIA IKIFANYA USHENZI, ITAPATA JIBU KALI

Televisheni ya al-Manar ya nchini Lebanon imemnukuu Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akisema kuwa iwapo Saudi Arabia itachukua hatua yoyote ya kipumbavu dhidi ya Iran, hakuna sehemu yoyote ya nchi hiyo itakayokuwa salama isipokuwa miji mitakatifu ya Makka na Madina tu.
Al-Manar imemnukuu Brigedia Jenerali Hussein Dehqan, Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran akiionya Riyadh kuwa, kiburi cha watawala wa Saudia kimewapelekea kutamka maneno ambayo wao wenyewe hawatambui uzito wake na kwamba kubwa zaidi wanaloweza kulifanya ni kuuchochea utawala haramu wa Israel dhidi ya Iran.
Waziri wa Ulinzi wa Iran amesema hii leo Saudia imekata tamaa kiasi cha kuifanya ijidhalilishe na kumsifu Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel. Hakuna wakati wowote ambapo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa na nia ya kuteka au kuichokoza nchi nyingine lakini imekuwa ikitangaza mara kwa mara kwamba haitasita kutoa jibu dhidi ya mchokozi yeyote na kwamba ina nguvu za kutosha za kuweza kuepusha vitishio na pia kutoa jibu kali la majuto dhidi ya adui mchokozi.
Nembo ya televisheni ya al-Manar ya Leanon
Watawala wa Saudia ambao wameutumbukiza ulimwengu mzima wa Kiislamu katika lindi la vita, machafuko na fikra za kuchupa mipaka badala ya kukiri makosa yao wameanza kuitisha Iran kwa vitisho ambavyo vyenyewe ni vikubwa kuliko uwezo wao. Kizazi kipya cha watawala wa Saudia kinyume na walivyokuwa watangulizi wao ambao kidogo walikuwa wakitahadhari katika kukabiliana na masuala ya eneo, kimeamua kwa pupa kuwa mstari wa mbele wa kukabiliana na masuala hayo bila ya kuchukua tahadhari yoyote ya lazima. Kizazi hicho ambacho kinaoongozwa na Muhammad bin Salman, Naibu Mrithi wa Kiti cha Ufalme na ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa Saudi Arabia kinaamini kwamba nchi hiyo inapasa kuwa na nafasi yake halisi katika eneo kwa kuchukua hatua za kijasiri na kishujaa zaidi. Kutumwa wanajeshi wa Saudia nchini Bahrain kwa ajili ya kuwakandamiza Mashia wa nchi hiyo, uvamizi wa nchi hiyo huko Yemen kwa ushirikiano wa Marekani na utawala ghasibu wa Israel, maafa ya Mina katika msimu wa Hija na kuuawa kidhulma Sheikh Nimr, mwanazuoni mashuhuri wa Saudia ni ishara zinazobainisha wazi utambulisho halisi wa watawala hao wapya wa ukoo wa Aal Soud. Muhammd bin Salman amethibitisha wazi kwamba kwa msingi wa sera mpya za Saudi Arabia za kufuatilia siasa za hujuma, anataka kulitwisha eneo hili fikra kwamba Riyadh ndiyo nguvu kubwa zaidi katika eneo hili la Mashariki ya Kati.
Brigedia Jenerali Hussein Dehqan
Utangazwaji wa uwepo huo wa nguvu wa Saudia unakamilishwa na hatua ya Bin Salman ya kujiunga na kambi ya Marekani, Uingereza na utawala haramu wa Israel katika eneo. Hii ni katika hali ambayo Saudia inakabiliwa na migogoro chungu mzima ya kisiasa, kiuchumi na kiusalama ambayo inaweza kusambaratisha kirahisi nguzo zilizozeeka za utawala wa kifalme nchini humo. Mbali na hayo sehemu kubwa ya siasa za Saudia zimesimama juu ya msingi wa kuudhaminia usalama utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo hili muhimu la Mashariki ya Kati. Pamoja na huduma hiyo yote kwa utawala huo haramu, lakini watawala wa Riyadh bado wana wasiwasi wa kuendelea kuitegemea Marekani kupita kiasi na kwa hivyo wameamua kuanzisha chokochoko na kubuni mbinu mpya za kubadilisha hali ya mambo katika eneo. Lakini ukweli wa mambo ni kuwa mfumo wa kisiasa wa Saudi Arabia umeshindwa kuendana na matukio ya hivi sasa ya kieneo na kimataifa na hivyo kushindwa siasa zake za uingiliaji katika eneo.
Bin Salman akiwa na Rais Trump wa Marekani
Pamoja na hayo lakini bado watawala wa Saudia wanadhani kwamba wanaweza kufidia nafasi yao iliyodhoofika katika eneo kwa kuanzisha siasa za uchokozi, uhasama na hujuma dhidi ya nchi nyigine, jambo ambalo bila shaka ni ndoto tu. Kile wanachopasa kukifahamika vyema watawala wa Saudia kimebainishwa wazi na Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sentensi fupi lakini iliyobeba ujumbe mzito, aliyoitakamka wakati wa kuhojiwa na televisheni ya al-Manar ya nchini Lebanon. Hivyo basi kama kizazi kipya cha watawala wa Saudia kitakuwa na chembe ya busara bila shaka kitalazimka kutafakari na kufahamu vyema iliko nafasi yake katika eneo, kwa sababu hata mabwana zao yaani Marekani na Israel hawana uwezo wa kuishambulia Iran. Hii ni kwa sababu wakiamua kuchukua hatua yoyote ya kipumbavu na kishenzi bila shaka watatumbukia kwenye shimo refu lisilo na kina ambapo itawawia vigumu kujinasua humo.

0 comments: