UN: WATU 4, 600 WANAKIMBIA MAKAZI YAO KILA SIKU NCHINI KONGO DR

Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakabili raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kupitia taarifa uliyotoa mjini Geneva, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa kila siku maelfu ya watu wanalazimika kuyahama makazi yao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kwa mujibu wa ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) hadi mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu watu milioni tatu na laki saba walikuwa wamebaki bila makazi nchini humo, idadi ambayo ni ongezeko maradufu kulinganisha na watu milioni moja na laki sita waliokabiliwa na hali hiyo mwanzoni mwa mwaka uliopita wa 2016.
Hali mbaya ya kibinadamu wa wakimbizi wa DRC
Rein Paulsen, mkuu wa OCHA nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva kuwa hali ya kibinadamu katika mkoa wa Kasai ulioko katikati mwa nchi hiyo ni mbaya zaidi na kuongeza kuwa machafuko na mapigano yaliyotokea kuanzia mwezi Septemba mwaka jana hadi sasa baina ya vikosi vya serikali na wanamgambo wa kikabila yamesababisha watu milioni moja laki mbili na elfu 70 kuyahama makazi yao.../

0 comments: