WAKENYA WASHINDA MBIO ZA BOSTON

Mkenya Geoffrey Kirui ameshinda mbio za 121 za Marathoni za Boston jana, akimshinda Galen Rupp wa Marekani ambaye ni mshindi mara tatu wa mbio hizo. Mkenya mwingine Edna Kiplagat alishinda pia mbio hizo kwa upande wa wanawake kwa kumpita dakika za mwisho Rose Chelimo, mzaliwa mwingine wa Kenya ambaye kwa sasa anapeperusha bendera ya Bahrain. Wanariadha wa kimarekani walishika nafasi mbili kati ya nne bora upande wa wanawake na sita kati ya kumi bora kwa upande wa wanaume. Katika soka, baada ya kupoteza mechi nne mfululizo nje ya uwanja wao katika ligi kuu nchini Uingereza, hatimaye Arsenal iliweza kupata ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Middlesbrough inayokabiliwa na kitisho kikubwa cha kushuka daraja.

0 comments: