TULIFUNGWA VITAMBAA USONI NA PINGU MIKONONI: ROMA MKATOLIKI AZUNGUMZIA MACHUNGU WALIYOWAKUTA

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa, maarufu kama Roma Mkatoliki, amewaambia waandishi wa habari waliofurika kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Saam leo Aprili 10, 2017 kuwa yeye na wenzake walitekwa na kufungwa vitambaa usoni na kufungwa pingu kula vipigo, kabla ya kutupwa ufukweni mwa bahari jijini Jumamosi "Tulipokuwepo si pazuri, tuliteswa na kupigwa  tulipiga alama ya msalaba na wenzetu wenye imani nyingine waliomba kwa dini zao." Alisema Roma, ambaye alikuwa na mkewe na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wenzake watatu aliotekwa nao pamoja na uongozi wa studio za Tongwe Records. Kwa upande wake, waziri Mwakyembe amewahakikishia watanzania kuwa watulifu na kwamba."
Lazima upelelezi kamilifu ufanyike tujue nini kimefanyika vinginevyo vitendo hivi vitaemdelea.” Alisema Dkt. Harrison Mwakyembe
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam
Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake pamoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe Records iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujumla kwakuwa inaonesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea , kushoto ni Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe.
 
Roma Mkatoliki akifafanua zaidi kwa waandishi wa Habari
Roma akiwaonesha wana habari namna alivyojeruhiwa aliokuwa akiteswa na hao watekaji ambao mpaka sasa hawajajulikana ni akina nani,kufuatia Uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam, Roma ameiomba serikali kuwahakikishia ulinzi wasanii pamoja na watanzania kwa ujula kwakuwa inaoyesha hawana usalama kabisa kutokana na tukio lenyewe lilivyowatokea. Kushoto ni Mke wa wa Msanii huyo, Bi Nancy.
Baadhi ya Wana Habari wakimsubiri msanii wa Muziki wa Kizazi kipya ajulikanae kwa jina la Roma Mkatoliki kuja kuzungumza nao na kuwaeleza kilichowatokea 
Baadhi ya Wana habari wakifuatilia tukio hilo 
Waziri wa habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akimsikiliza kulia Msanii wa bongo Fleva kutoka Tanzania Ibrahim Musa aka Roma Mkatoliki akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jioni hii wakati akizungumzia sakata la kutekwa kwake paoja na wasanii wenzake katika studio ya Tongwe iliyopo Masaki jijini Dar es salaam 

Mke wa Roma Mkatoliki Nancy (mwenye kilemba cha bluu) pamoja na baadhi ya wasanii wakisubiri kuanza kwa mkutano huo wakati Msanii huyo akijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata la kutekwa kwake kulia ni Waziri wa Habari , Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe. 
Waziri wa habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dk. Harisson Mwakyembe akiongozana na wasanii Roma Mkatoliki na wenzake ili kuzungumzia sakata la Roma Mkatoliki lililotokea hivi karibuni.

0 comments: