SERIKALI KUKAMILISHA MKAKATI WA TAIFA WA MIAKA MITANO WA KUPANDA MITI

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kushirikiana na wadau iko katika hatua za mwisho kukamilisha Mkakati wa Taifa wa miaka mitano wa kupanda na kutunza Miti nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)Mhe.Luhaga Mpina wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge leo Mjini Dodoma.

“Tunaitaji kiasi cha shilingi bilioni 105 ambapo kila mwaka tutatenga  bilioni 20 kutoka vyanzo mbalimbali vya Serikali na wadau wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati huu ambao unaelekeza kila mwananchi,Taasisi za Serikali,Taasisi za madhehebu,Asasi zisizokuwa za Serikali,kambi za Majeshi,Magereza,Shule na makampuni kupanda na kutunza miti katika maeneo yao”,Alisema Mhe.Mpina.

Aidha amesema kuwa mkakati huu ni tofauti na mikakati mingine iliyopita kwani kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini itahakikisha kwamba miti inayopandwa inatunzwa na kukua na kuhakikishia visababishi vinavyochangia miti kutokuwa vimebainishwa na mikakati ya kuvidhibiti imeandaliwa ikiwa ni pamoja na upandaji wa aina  ya miti kulingana na maeneo na utunzanji wa miti hiyo.

Hata hivyo Serikali imekuwa ikitekeleza zoezi la upandaji miti kote nchini kupitia Ofisi hii ambapo kila halmshauri inatakiwa kupanda miti 1,500,000 kila mwaka na kuhakikisha inatunzwa nna pale itakapoonekana inafaa Halmshauri zihahakishe maeneo ya wazi yanahifadhiwa ili kuruhusu uoto wa asili kurejea.

0 comments: