KOREA KASKAZINI: TUTAFANYA MAJARIBIO YA MAKOMBORA KILA WIKI


Korea Kaskazini itaendelea kufanya majaribio ya makombora yake, Afisa wa juu nchini humo ameiambia BBC mjini Pyongyang, ingawa jamii ya kimataifa imekuwa ikikemea majaribio hayo.

''Tutatekeleza majaribio zaidi katika kipindi cha kila juma,kila mwezi na kila mwaka," alieleza makamu waziri wa masuala ya kigeni Han Song-ryol alipokuwa akizungumza na mwanahabari wa BBC, John Sudworth.

Awali, Makamu wa rais wa Marekani, Mike Pence aliionya Korea kutoijaribu Marekani, akisema kuwa muda wa kuivumilia nchi hiyo kwa miaka mingi umekwisha.

Bwana Pence aliwasili mjini Seoul nchini Korea Kusini mwishoni mwa juma lililopita baada ya Kombora la Korea kaskazini kushindwa kupaa.

Hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka katika eneo la Peninsula, wakati huu kukiwa na hali ya kushambuliana kwa maneno baina ya Korea kaskazini na Marekani.

Bwana Han ameiambia BBC: ''Ikiwa Marekani inapanga kutekeleza shambulio la kijeshi dhidi yetu tutachukua hatua ya kupambana kwa shambulio la Nuklia kwa mbinu zetu na mtindo wetu.

0 comments: