JESHI LA YEMEN LAENDELEA KUPATA MAFANIKIO DHIDI YA VIBARAKAWA SAUDIA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:41 AM
Askari wa serikali ya Yemen kwa kushirikiana
na Harakati ya Wananchi ya Answarullah limeendelea kupata mafanikio
katika operesheni kadhaa lilizozifanya katika mikoa ya Lahij, Dhale na
Taiz na kufanikiwa kuwaangamiza askari wengi vibaraka wa Saudia sambamba
na kuwatia hasara kubwa.
Taarifa iliyotolewa na jeshi la
Yemen imesema kuwa, askari wa serikali na harakati hiyo ya Answarullah,
wameweza kuwazuia askari vamizi wa Saudia na waungaji mkono wao kuelekea
mji wa Kirsh mkoa wa Lahij, kusini mwa Yemen ambapo kumejiri mapigano
makali yaliyowafanya askari wa Saudia kurudi nyuma na kukimbia.
Hii ni katika hali ambayo kikosi cha
mizinga cha jeshi na harakati ya Answarullah kilichopewa jina la
'al-Swaderain' kimelilenga eneo la 'Maris' la mkoa wa Dhale, kusini mwa
nchi ambapo kumewekwa kambi ya jeshi la askari wa Saudia na kufanikiwa
kuangamiza baadhi yao. Kadhalika magari kadhaa ya kijeshi ya Saudia
yaliyokuwa yamewabeba askari wa nchi hiyo vamizi wameangamizwa huko
magharibi mwa mkoa wa Taiz. Makumi ya askari wa Saudia na vibaraka wake
wameangamizwa katika siku za hivi karibuni katika maeneo tofauti ndani
na nje ya Yemen na hivyo kuitia hasara kubwa Saudi Arabia na washirika
wake.
Wakati huo huo duru za kuaminika zimeripoti kuibuka mapigano makali
baina ya askari wanaomuunga mkono Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani
wa Yemen aliyejiuzulu na kutoroka nchi. Kwa mujibu wa ripoti hiyo,
mapigano hayo yametokea huko mkoa wa Aden, baada ya kundi moja kati ya
askari hao kutaka kudhibiti kituo cha upekuzi mkoani hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: