BASI LATUMBUKIA MTONI-UVINZA -KIGOMA

NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA

ABIRIA kutoka  Vijiji vilivyopo mwambao mwa  Ziwa Tanganyika Mkoa wa Kigoma wamebaki njia panda kuelekea kigoma mjini na wengine hawajui hatma ya mizigo yao,baada ya   basi walilokuwa wamepanda linalofanya shughuli ya usafirishaji kutoka Sigunga kwenda Kigoma mjini  la Saratoga kutumbukia katika mto ilagala  uliopo  wilaya ya Uvinza.


Akifafanua hilo Shuhuda wa ajali hiyo,Mwenyekiti wa SACCOS Kijiji cha Ilagala Abdallah Mpolwe alisema wakiwa katika shughuli zao za kawaida pembezoni mwa kivuko hicho,waliona kivuko cha Mv-Ilagala kikiwajibika,ilipotia nanga ndipo basi hilo la abiria linalotoa huduma ya usafiri kutoka Sigunga kwenda kigoma Mjini la Saratoga likitoka  ndani ya  kivuko hicho,lakini ghafla  basi hilo lilirudi nyuma na kutumbukia mtoni.

Alisema  Novemba ,23, mwaka huu saa 2.30 asubuhi ndipo ajali hiyo ilitokea ambapo chanzo cha ajali  ni kushindwa kwa breki la basi hilo lenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 60,baada ya kushindwa  kupandisha barabara kutoka ilipotia nanga kivuko ,na  nchi kavu na  kukiri hakuna abiria aliyekufa japokuwa inasemekana kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye alibaki humo kutokana na maradhi aliyokuwa akiugua .

Kwa mujibu wa mmoja wa nahodha wa kivuko hicho jina hifadhini  kwa usalama wa mahusiano na wadau wa kivuko hicho alisema baada ya kutia nanga ,dereva aliondoa basi katika kivuko hicho kama kwaida yake lakini kwa bahati mbaya gari ilishindwa kupanda mlima wa barabara husika hatimaye ilirudi kinyumenyume hatimaye kutumbukia  mtoni huku dereva akiwa hai.

Jamboleo lilipiga hodi ofisini kwa  Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma  Ferdinand Mtui alipohojiwa  juu ya ajali hiyo alisema wanasubiri utaratibu kutoka kwa mmiliki wa mabasi ya Saratoga kwa ajili ya kwenda kijiji cha ilagala katika kivuko cha mto huo kushuhudia uhalisia wa mambo na kuahidi kutoa tarifa kamili baada ya kutoka katika eneo la tukio.
Mwisho.

0 comments: