UN NA SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI ILIYOPO NCHINI

IMG_0482
Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Nyanza jijini Mwanza kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani ambapo kitaifa yamefanyika jijini humo na kuandaliwa na Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania (IRCPT) kwa ushirikiano wa UNESCO ambapo yaliwashirikisha Viongozi wa Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Viongozi wa madhehebu ya dini, Jeshi la Polisi, Walemavu, Wananchi pamoja na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi na wa pili kulia ni Afisa Mfawidhi Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kanda ya ziwa Mwanza, Bw. Ludovick Ringia.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).


Na Modewjiblog team, Mwanza
Umoja wa Mataifa (UN) umesema utaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kulinda na kudumisha amani ya pamoja kwa makundi yote ili amani iliyopo itumike kuleta maendeleo endelevu nchini.
Hayo yamebainishwa na Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues, wakati akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Amani Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza (Septemba 21.2015).
Bi.Rodgrigues amesema amani ya pamoja inatoa nafasi kwa kila mmoja kuwa mshirika wa kudumisha na kuendeleza amani bila kujali itikadi, imani au matabaka mbalimbali yaliyipo ndani ya jamii.
Amefafanua kuwa Tanzania ni mfano wa kuigwa katika kulinda amani, hivyo nguvu ya pamoja ni muhimu katika kufikia malengo na maendeleo yanayotakiwa kutokana na kuwepo kwa utulivu, mshikamano, umoja, na amani.
Kwa upande wake, Msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amewataka watanzania kuachana na propaganda za kisiasa zinazoleta chuki na hasa katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Jaji Mutungi ameeleza kuwa amani haina tabaka na kusisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura kwa kutumia falsafa ya kulipenda taifa na kuwaonya viongozi wa vyama vya siasa kuacha kuwadharau watanzania ambao wameilinda amani kwa muda mrefu.
Nalo Jeshi la Polisi mkoani humo, limelaani kitendo kilichofanywa na watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa vyama vya siasa kwa kushambulia polisi na kuvunja vioo vya gari la polisi kwa kusingizio cha kampeni za uchaguzi.
Katika tukio hilo imeelezwa kuwa, baada ya watu waliokuwa wakitokea katika mkutano wa kampeni wa umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) kushambulia Polisi, kuvunja vioo vya gari la polisi na kujeruhi askari.
IMG_0627
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye maadhimsho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kilele hicho cha siku ya Amani jijini hapa.
Kamanda Mkumbo ameeleza kuwa kitendo hicho ni uhalifu kama uhalifu mwingine na polisi haiwezi kuvumilia vitendo vya aina hiyo na hasa wakati huu ambapo kampeni za uchaguzi zinaendelea.
Maadhimisho ya siku ya amani duniani yanafanyika septemba 21, kila mwaka ili kukumbuka na kulinda amani na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Amani Kwanza – Utamaduni wetu wa amani ni nguvu yetu”. Ambapo siku hiyo pia viongozi mbalimbali waliweza kuhudhuria siku hiyo wakiwemo viongozi wa siasa, dini, jeshi la Polisi, viongozi wa serikali na binafsi pamoja na wananchi mbalimbali.
IMG_0867
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akitoa ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Unesco, Irina Bokova kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
IMG_0762
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
IMG_1018
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akitoa nasaha zake kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.
IMG_0701
Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
IMG_1297
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo akiteta jambo na Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani, ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
IMG_1375
Kikundi cha kwaya ya Patimo-Mabatini jijini Mwanza kikitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
IMG_1312
Burudani ya Qaswida maalum iliyobeba ujumbe wa kutunza 'Amani' ikitolewa.
IMG_1484
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga akiweka saini kwenye Azimio maalum la kuenzi Amani lililoandaliwa kwenye maadhimisho hayo huku Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania (IRCPT), Rev. Canon Godda (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.
IMG_1502
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo (kushoto) na viongozi mbalimbali wa dini wakiendelea kusaini Azimio hilo.
IMG_1537
Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akiweka sahihi kama shuhuda katika kupitisha Azimio hilo.
IMG_1553
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi naye akiweka saini kama shuhuda wa kupitisha Azimio hilo. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga.
IMG_0584
Pichani juu na chini ni makundi ya Viongozi mbalimbali wa madhehebu ya dini, Viongozi wa Serikali, Asasi za Kiraia, Waandishi wa habari, Jeshi la Polisi na Walemavu waliodhuruia siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Shule ya msingi Nyanza.
IMG_0591
IMG_0595
IMG_1426
IMG_1473
Wawakilishi wa vikundi vya vijana walioshiriki maadhimisho ya siku ya Amani Duniani ambayo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza.
IMG_1061
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya msingi Nyanza walikuwa ni miongoni mwa washiriki wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani duniani.
IMG_1563
Meza kuu katika picha ya pamoja.
IMG_1583
Washiriki katika picha ya pamoja na meza kuu.
IMG_1592

0 comments: