Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashimu Rungwe, amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza nchi kitahakikisha kinawaondoa wakuu wa mikoa na wilaya, na kuanzisha serikali ya majimbo.
Akizungumza jana kwenye kampeni zake za kuwania urais, uliofanyika kwenye kituo cha mabasi ya zamani mjini Shinyanga, Rungwe alisema wakuu wa wilaya na mikoa wamekua kero kwa wananchi kwa kuwa hawachaguliwi bali wanateuliwa na rais, na kwamba wamekuwa wakitumikia sera ya chama hicho kilicho wachagua.
Sera ya Chaumma kama tutapa ridhaa ya kuongoza Serikali ya Tanzania lazima tutawaondoa wakuu wa mikoa na wilaya, kwani ndio watu wanaochangia wananchi kutokuwa na maendeleo na kubaki na wimbi la umaskini,î alisema Rungwe na kuongeza kuwa.
Viongozi hawa wamekuwa wanafanya wanavyotaka kwa sababu wananchi hawajawaweka kwenye nafasi hizo, Sasa Chaumma itaanzisha serikali ya majimbo vyama vyote vishiriki kugombea nafasi hizo, kwa kufanya hivyo watawathamini wananchi, kwani wao ndio watakua wamewaweka madarakani na wanauwezo wa kuwaadhibu.
0 comments: