Na Andrew Carlos/GPL
WASANII
wengi ambao wanaamini wana uwezo mkubwa wa kuigiza, wamejitokeza leo
ndani ya Isamilo Lounge kufanyiwa usaili katika lile shindano la kusaka
vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT).
Akizungumza
na mtandao huu, msemaji mkuu wa shindano hilo, Happiness Ntanga alisema
kuwa wanashukuru kwa Kanda ya Ziwa kupokelewa vizuri ambapo wengi
wameguswa na shindano hilo.
“Niwaambie
tu, usaili huu tutaendelea nao mpaka Jumatano ya Aprili 29 na baada ya
hapa tutaelekea Kanda ya Kaskazini yaani Arusha hivyo wote wenye vipaji
mjiandae,” alisema Ntanga.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ni Mpaka Kieleweke ambapo Mei 6, mwaka huu kutakuwa na
uzinduzi wa filamu iliyojumuisha wale wakali walioingia 10 bora msimu
wa kwanza.
0 comments: