Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:17 PM
Mrakibu wa Polisi-Captain Kidai Senzala Kaluse enzi za uhai wake.
Familia
ya Mzee Senzala Kaluse wa Kimara Mwisho Dar es Salaam, inasikitika
kutangaza kifo cha mtoto wao KIDAI SENZALA KALUSE kilichotokea Novemba
29, 2014 Saa 4 asubuhi kwa ajali ya Helkopta huko Kipunguni B, Moshi Bar
Dar es Salaam.
Mipango
ya mazishi inafanyika nyumbani kwa baba yake Mzee Kaluse, Kimara Mwisho.
Habari ziwafikie, Ukoo wote wa Warutu, Ukoo wa Kaluse, Ukoo wa Mroki,
Familia yote ya Timothy Nathan, Ukoo wa Kajiru na Taluka, Wakamba wote
wa Ugweno Msangeni, Bibi wa Marehemu Mary Nathan wa Kinyenze- Morogoro, Familia ya Tarimo ya Ukonga Mombasa, Omary Msuya wa Moshi, Abdalh Mgonja wa Gonja Maore, Hosea wa Arusha.
Taarifa
pia ziwafike maofisa wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Kikosi cha
Polisi Anga, Ndugu, Jamaa na Marafiki popote pale walipo.
Misa ya
kuaga Mwili wa Marehemu itafanyika mnyumbani kwao kuanzia Saa 6:00 kabla
ya safari ya kuelekea Gonja Maore, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro
kuanza na mazishi yatafanyika Jumatatu Kijijini Kwao Gonja Maore.
Mawasiliano zaidi: Mroki Mroki- +255 717002303.
MATAYO 5: 4 HERI WENYE HUZUNI; MAANA WAO WATAFARIJIKA
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:12 PM
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA 3 WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI (EAC) KUHUSU MIUNDOMBINU JIJINI NAIROBI, KENYA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
wa tatu kutoka (kushoto) Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto, (kushoto
kwake) Makamu wa Rais kwanza wa Burundi, (kulia kwake) wakijumuika kwa
pamoja na viongozi wengine wakionyesha Taarifa ya pamoja waliyoisaini
kuhusu majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa Nchi za
Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika kwenye Ukumbi wa
KICC, jijini Nairobi jana Novemba 29, 2014.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza katika mkutano wa 3 tatu wa wakuu wa Nchi za Afrika
Mashariki (EAC) kuhusu miundombinu, uliofanyika katika ukumbi wa KICC
jijini Nairobi jana.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini taarifa ya pamoja ya majadiliano ya kuimarisha Miundombinu kwa
nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati wa mkutano wa 3 wa
Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu jijini
Nairobi, Kenya jana.

Baadhi ya washiri wa mkutano huyo kutoka nchini Tanzania......

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiongozana na baadhi ya viongozi wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa
mikutano wa KICC, baada ya kushiriki katika mkutano wa 3 wa Wakuu wa
Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu uliofanyika jijini
Nairobu, Kenya jana.

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika
mkutano huo.

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia jambo na Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto na Waziri wa
Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wakati wakiondoka katika viwanja vya
Ukumbi wa mikutano wa KICC, baada ya kushiriki kwenye mkutano wa 3 wa
Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) kuhusu Miundombinu, uliofanyika jijini Nairobi, Kenya jana.
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:07 PM
MSICHANA WA KAZI ALIYEMPIGA MTOTO AFUNGUKA MAZITO!

ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:05 PM
HABARI MBAYA KWA MASHABIKI WA MANCHESTER UNITED LICHA YA KUSHINDA KWA KISHINDO JANA!
Unapozungumzia suala la majeraha ya wachezaji bila shaka mashabiki wa Manchester United wanapata homa ya ghafla .
Hii ni kwa sababu timu hii imekuwa na orodha isiyoisha ya wachezaji wenye majeraha .
Mbaya zaidi ni kwamba kila orodha hii inapoonyesha dalila za kungua mchezaji mwingine anaemia na inazidi kuwa ndefu .
Orodha hii iliongezeka kwenye mchezo dhidi ya Hull City wakati ambapo
kiungo mshambuliaji Angel Di Maria alipoumia misuli ya nyonga kwenye
dakika ya 14 ya mchezo na kulazimika kutoka.
Bado haijafahamika Di Maria atakaa nje ya uwanja kwa muda gani lakini
kwa kawaida jeraha kama hili huhitaji kati ya siku 7 mpaka 10 ili
kupona na wakati mwingine kuendana na ukubwa wake linaweza kuhitaji muda
mrefu zaidi .
Kwa jumla Jeraha la Di Maria ni jeraha la 41 kwa mchezaji wa
Manchester United kwa msimu huu tangu kuanza kazi kwa kocha Mholanzi
Louis Van Gaal .
Idadi hii ndio idadi kubwa ya majeraha kwa wachezaji kwa timu yoyote
ya ligi kuu ya England msimu huu hali inayowafanya United waamini kuwa
huenda timu yao ina mkosi wa aina Fulani.
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:03 PM
WATOTO WA RAIS OBAMA NDANI YA SKENDO CHAFU YA MAVAZI YA KIHASARA!
Rais
Barrack Obama na wanawe Sasha na Malia. Afisa mmoja wa chama cha
Republican amewakosoa mavazi yao.Watoto wa rais wa Marekani Barrack
Obama, Sasha na Malia wameshtumiwa kwa kukosa heshima na afisa mmoja wa
chama cha Republican baada ya kuhudhuria sherehe za kutoa shukrani.
Elizabeth Lauten ,ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano wa mbunge
Stephen Fincher alitoa matamshi yake katika mtandao wa facebook ambayo
baadaye yalifutwa.
Aliku akikosoa sketi fupi zilizovaliwa na wasichana hao wa Obama.Bi
Lauteni pia aliwashtumu wasichana hao kwa kuonyesha uchovu wakati
waliposimama na baba yao katika sherehe hiyo ya ikulu ya Whitehouse.
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
9:01 PM
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
8:34 AM
BUNGE LAHIRISHWA TENA ASUBUHI HII
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Anne Makinda akifafanua jambo wakati akiendesha Bunge hilo
Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Anna Makinda Amelazimika Kuliahirisha Bunge Asubuhi Kwa mara ya Pili mara baada ya Kuliahirisha Saa tatu Asubuhi Hadi saa Kumi Jioni .
Hali hiyo Imetokana na Mazungumzo yanayoendelea kwajili ya Wabunge Kuridhiana Maendekezo ya Kamati ya PAC yaliyokuwa yanataka Baadhi ya Viongozi Kuwajibika.Hali iliyosababisha Bunge hilo kutokuelewana la Kulazimika Kuhairishwa jana Saa nne Usik

8:31 AM
RAIS KIKWETE AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI MARA BAADA YA KUTUA LEO AKITOKEA MAREKANI KWENYE MATIBABU
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
5:30 AM
BI HARUSI JESCA TITUS NDIBOHOYE MUDA SI MREFU ANATARAJIA KUFUNGA PINGU ZA MAISHA NA EDWIN MOSES.
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 5:07 AM
Bi Harusi mtarajiwa Jesca Titus Ndibohoye , katika Pozi baada ya kupambwa tayari kwenda kufunga pingu za Maisha na Bwana Harusi Edwin Stephen Moses, katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es Salaam , Mtakatifu Clement Goba na kufatiwa na Hafla ya sherehe yao itakayo fannyia katika Ukumbi wa Lounge uliopo King'ongo kwa Komba Goba (PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Bi Harusi katika Pozi baada ya kupambwa leo , kwenda kufunga Pingu za maisha na Bwana Edwin Moses, katika Kanisa la Angikana Kigango cha MT. Clement Goba leo.
Taarifa
kutoka mjini Kano, Kaskazini ya Nigeria, zinasema kuwa watu wengi
wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la bomu.
Ni
baada ya milipuko mitatu inayoaminika kuwa ya mabomu kutokea katika
msikiti mkubwa zaidi mjini humoulio katikati mwa jiji karibu na eneo
anakoishi Emir au kiongozi wa waisilamu nchini humo Muhammad Sanusi.Emir huyo kwa sasa yuko nchini Saudi Arabia.
Mabomu hayo yalilipuka wakati maombi ya Ijumaa yalipokuwa yanaendelea.
Mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, alihesabu karibu miili 50 ya waliofariki katika shambulizi hilo.
Taarifa zingine zinasema watu waliokuwa wamjihami waliaingia msikitini humo na kuanza kufyatua risasi baada ya mabomu kulipuka.
Wapiganaji wa Boko Haram, wamekuwa wakifanya mashambulizi katika mji huo ambao ni mkubwa zaidi Kaskazini ya Nigeria.
Mapema mwezi huu , Emir alitoa wito kwa watu kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayofanywa na Boko Haram.
Aliwashauri wakazi kujihami na kufanya kila wawezalo kujikinga dhidi ya mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo.
Msemaji wa Polisi alisema matamshi ya Emir, yalikuwa ya uchochezi na kwamba watu wanapaswa kumpuuza.
Mtoto X amelala kwa utulivu, akiwa
amefunikwa na Blanketi lenye kumpa joto na kukumbatiwa na Mama yake
katika Nyumba moja ya kulelea Watoto yatima nchini Kenya.
Mtoto
huyu ni wa miezi miwili hivi sasa, alizaliwa kufuatia tendo la ngono
kati ya msichana na Mjomba wake, mtoto huyu anaelezwa kupatikana katika
mazingira ya miiko.Katika nyumba ya watoto wa Kanduyi, mjini Bungoma magharibi mwa Mji wa Nairobi, kama ilivyo kwa Watoto wengine , Mtoto huyu aliokolewa kutoka kwenye Familia yake kulipokua na mipango ya kuuawa.
Katika tukio hilo,siku mbili tu baada ya kuzaliwa Mtoto X, baada ya kupewa Taarifa vikosi vya usalama vilivamia makazi ya mtoto huyo na kumchukua wakiyaokoa maisha yake kutokana na kifo kilichokuwa kinamkabili mbele yake, kifo kilichaoamriwa na wazee wa kimila wa jamii iitwayo Bukusu.
Kuna watoto kama yeye katika nyumba hii ya Kunduyi wenye umri kati ya siku moja mpaka miaka 18.
Watoto waitwao 'mwiko'
Kujamiiana kwa maharimu ni mwiko nchini Kenya kama ilivyo katika maeneo mbalimbali, kwa mujibu wa Sheria ya Kenya, hilo ni kosa lenye kuadhibu kwa kifungo cha miaka mitano,au kifungo cha maisha kwa kujamiiana na binti wa umri mdogo
Lakini kwa Karne nyingi, adhabu ya kimila katika Jamii nyingi za Kenya ni kifo,na katika jamii ya Bukusu si lazima Mwanaume na Mwanamke waliohusika, lakini pia mtoto atakayezaliwa kutokana na uhusiano ulio mwiko.
Waziri wa utamaduni katika Kaunti ya Bungoma,Stephen Kokonya amesema kumekuwa na mahusiano ya namna hii yameenea katika jamii na kuongeza kuwa si sheria kwa jamii kutoa adhabu ya kifo, ni Jaji pekee anayeweza kuhukumu.Kokonya amesema katika maeneo ya kijijini hii ni sehemu ya Sheria za kijamii watoto kuonekana kuwa wamelaaniwa.
Watu wa jamii ya Bukusu huwaita Watoto hawa ''be luswa'' wakimaanisha ''Watoto haram'' wakihofu kuwa watasababisha kupata laana kama utasa na magonjwa ya akili.
''Kila mara tunaposikia mtoto anayedaiwa kuwa haramu amezaliwa katika eneo lolote huwa tunakimbia upesi kumuokoa vinginevyo unaweza kufika na kuambiwa tayari Mtoto alishakufa''Afisa anayetunza Watoto katika nyumba ya Watoto wa Kanduyi,Alice Komotho ameiambia BBC.
Kokonya amesema Serikali inatoa elimu ya uelewa kuhusu vitendo vya adhabu zitolewazo kinyume cha sheria ya nchi na Wazee wa jamii ya Bukusu.
Kisa cha Msichana.
Mama wa miaka 15 ambaye mtoto wake aliokolewa amerudi shuleni,binti huyu wa miaka 15 alibakwa na Mjomba wake. Msichana huyu amesema Mjomba wake alimtishia kuwa atampiga ikiwa atatoa taarifa kuhusu tukio la kubakwa, binti huyu alibakwa na mjomba wake mwenye umri wa miaka 17.
Msichana huyu hivi sasa amerudi shuleni kurudia mwaka wake alioupoteza alipokua mjamzito.
Binti huyu anaeleza kuwa hana mapenzi na Mjomba wake wala mtoto wao.
Mama huyu mdogo ameiambia BBC kuwa anapenda kuwa Daktari atakapomaliza masomo.
Maafisa wanasema kuwafundisha wazee wa kimila itakua ni njia nzuri ya kumaliza mila na desturi mbaya katika maeneo ya vijijini.
Mjomba wa Msichana huyo alikataa kuzungumza na BBC baada ya kuwasiliana nae.
Haki ya Kuishi
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wazee wa Bukusu anaeleza namna mtoto anavyouwawa,anakataa kuzungumzia kisa cha Mtoto X lakini anaeleza namna mtoto wanayedai kuwa haramu anavyouawa, anaeleza..
''Wakati binti anapokaribia kujifungua,huwakusanya baadhi ya Wanawake ambao hujifanya kama wanakwenda kumsaidia mzazi badala yake humziba pumzi mtoto kwa kuzibana nyonga za mama na kumuua Mtoto.
Wakinamama hawa hufanya haya kwa makini wakiamini kuwa ni budi mtoto kufa ili mzazi aishi katika jamii kwa amani.
Mzee mwingine anasema pia Wanakijiji wakati mwingine huua uzao wa pili ambao huwa pacha kwa madai kuwa huleta hali ya bahati mbaya, ambao wanapenda kubaki na watoto wao hulazimishwa kuondoka kijijini hapo.
Lakini Waziri wa utamaduni anasema kuwa angependa kuwakumbusha Wazee wote ambao hukaa na kuamua maamuzi ya mauaji kuwa wanaingilia haki ya msingi ya kuishi.
TIMU YA STAND MPYA. F C YAIFUNGA MABAO 8 - 1, TIMU YA Bantu ya IPULI ,ZOTE ZA MANISPA YA TABORA.
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:39 PM
Picha ya pamoja ya Timu ya Stand Mpya ya Babasi yaendayo Mikoani kabla ya Mtanange Dhidi ya Timu ya Bantu Fc ya Ipuli.(PICHANA KHAMISI MUSSA) Tabora
Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
11:37 AM
MPASUKO : ESCROW WABUNGE WAGAWANYIKA
Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati) akiwasihi Mbunge wa
Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa Nkasi, Ali Kessy
wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.
(Picha na
Emmanuel Herman)Dodoma. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali
(PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na
kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake
na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.
Juzi, kamati hiyo ya
Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo
amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba
ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma.
Kamati hiyo ilieleza
kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu
aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya
umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji.
Akiwasilisha
taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua
hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa
na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa.
Jana,
alieleza kuwa pendekezo la Kamati ya PAC kutaka mitambo ya IPTL
itaifishwe si sawa kwa kuwa kulingana na mkataba wa PPA kati ya Tanesco
na IPTL, majukumu ya IPTL yalikuwa ni kujenga, kumiliki na kuendesha
(Build, Own and Operate – BOO). Hivyo, kutaifisha mtambo huo ni kukiuka
makubaliano katika mkataba wa PPA wa Mei 26, 1995.
“Ukiukwaji wa
aina hii ukitokea unaweza kuingiza Serikali katika mgogoro mkubwa ikiwa
ni pamoja na kushtakiwa kwenye Mahakama za kibiashara za kimataifa.
Aidha, utaifishaji wa miradi ya uwekezaji binafsi itakuwa ni njia ya
kufukuza wawekezaji.”
Gharama za uwekezaji
Kuhusu taarifa
ya kamati ya PAC kwamba mwaka 2004 Tanesco ilifungua shauri katika
Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro ya Kiuwekezaji (ICSID 2)
kupinga kiasi kikubwa cha tozo ya gharama za uwekezaji, Profesa Muhongo
alisema suala hilo si kweli.
Alifafanua kuwa Tanesco haijawahi
kufungua shauri lolote ICSID ya London au Mahakama yoyote dhidi ya Benki
ya Standard Charterd kupinga kiasi kikubwa cha Capacity Charge kama
inavyoelezwa na PAC.
“Shauri la ICSID 2 lilifunguliwa Oktoba 31,
2010 na Standard Chatered Bank Hong Kong (SCBHK) kwa ajili ya kudai
malipo ya deni ililonunua kutokana na mkopo uliotolewa na mabenki ya
ushirika ya Malaysia kwa IPTL. Wahusika katika shauri hilo la ICSID 2 ni
SCBHK na Tanesco na wala siyo Tanesco na IPTL.”
Alisema
Februari 12, ICSID ilitoa uamuzi kuhusiana na shauri la SCBHK na Tanesco
na kuwashauri wakae kukokotoa upya malipo ya Capacity Charge. Hata
hivyo, ilikuwa vigumu kwa pande hizo kutekeleza uamuzi huo kutokana na
pande hizo kutokuwa na mkataba wa kibiashara baina yao.
“Vilevile,
kupitia shauri la madai Na. 60/2014, lililofunguliwa na IPTL katika
Mahakama Kuu ya Tanzania Aprili 4, ilizuia utekelezaji wa maelekezo
hayo,” alisema.
Uwekezaji wa Sh50,000
Profesa Muhongo
alisema kuhusu madai ya PAC kuwa mtaji wa uwekezaji katika mtambo wa
IPTL ni Sh50,000 na kwamba huo ndiyo ungetumika kukokotoa gharama za
uwekezaji ili kulipa tozo ndogo kuliko ilivyo sasa, maelezo hayo siyo
sahihi.
Alisema ukweli ni kwamba kutokana na uamuzi ya ICSID 1
ya Julai 12, 2001, gharama za ujenzi wa mtambo wa Tegeta ni Dola za
Marekani 127.2 milioni kama ilivyoelezwa na taarifa ya Mdhibiti na
Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Profesa Muhongo
alisema katika taarifa hiyo, pia imeelezwa kuwa ilikubalika kuwa uwiano
wa deni na mtaji utakuwa 70:30 ikiwa na maana kwamba, deni ni Dola za
Marekani 89.04 milioni na mtaji ni Dola za Marekani 38.16 milioni na
kwamba uamuzi huo haujabadilishwa na Mahakama yoyote au mtu yeyote.
“Tunakubaliana
kwamba fedha iliyopokewa kutoka mabenki ya ushirika ya Malaysia kama
mkopo ni Dola za Marekani 85.86 milioni ambazo kati ya Dola za Marekani
105 milioni zilizokuwa zimeidhinishwa,” alisema na kuongeza:
“Swali
la kujiuliza je, mtambo huo ulikamilikaje kwa gharama ya Dola za
Marekani 85.86 milioni, huku gharama halisi ya ujenzi wa mtambo wa
Tegeta ikawa Dola za Marekani 127.2 milioni?
Alisema ni dhahiri
kwamba kuna matumizi ya zaidi ya Dola za Marekani 38.16 milioni ambazo
pia zimetumika kwenye uwekezaji na kwamba Kamati ya PAC haikuonyesha
fedha hizo kuwa sehemu ya uwekezaji.
PAP na umiliki wa hisa saba
Profesa
Muhongo alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za Brela za Desemba 31,
2013, uhamishaji wa hisa saba za Mechmar katika IPTL kwenda PAP
ulisajiliwa hapa nchini. Kwa maana hiyo, PAP ni mmiliki wa asilimia 70
za IPTL. Alisema Kamati ya PAC imeeleza kuwa PAP siyo mmiliki halali wa
hisa saba za Mechmar katika IPTL lakini kamati imethibitisha kwamba
nyaraka za mauziano kati ya Mechmer na Piper Link zilipokewa na
Harbinder Singh Sethi ambaye pia ndiye mmiliki wa PAP.
“Kwa uthibitisho huo, kamati inakubali kuwa hisa za Mechmer katika IPTL zinamilikiwa na PAP,” alisema Profesa Muhongo.
Akana kuwa dalali
Profesa
Muhongo alisema taarifa ya Kamati ya PAC kwamba yeye ndiye aliyekuwa
dalali mkuu aliyewakutanisha Harbinder Sethi na James Rugemalira siyo
sahihi kuwa tangu Novemba 9, 2011, Rita iliitisha mkutano na
kuwakutanisha wadau wote wa IPTL wakati yeye alikuwa hajateuliwa kwenye
wadhifa huo.
“Mimi kama ni dalali, udalali wangu ni kupeleka
umeme vijijini. Mimi kama ni dalali udalali wangu ni kusaidia wachimbaji
wadogo wa madini na kupeleka Watanzania kusoma masters (shahada ya
pili) duniani kote.”
Serikali kutokuchukua tahadhari
Waziri
alisema Kamati ya PAC, imeeleza kuwa Serikali haikuchukua tahadhari ya
kutosha dhidi ya madai mengine yanayoweza kujitokeza kabla ya kutolewa
kwa fedha kutoka akaunti ya escrow kitu ambacho alidai si kweli.
Profesa
Muhongo alisema kinga iliyochukuliwa inakidhi matakwa ya kisheria na
imezingatia athari yoyote ambayo ingeweza kutokea baadaye kutokana na
kutolewa kwa fedha katika akaunti ya escrow.
“Kwa hiyo, siyo kweli kwamba Serikali haikuchukua tahadhari kama ilivyodaiwa na PAC.”
Madai ya Sh321 bilioni
Profesa
Muhongo alisema hoja ya PAC kwamba imejiridhisha kuwa madai ya Tanesco
ya Sh321 bilioni yana uhalali japo usahihi wake utapatikana baada ya
kutekelezwa kwa uamuzi wa ICSID 2 na Tanesco na IPTL kukubaliana kiwango
sahihi cha Capacity Charge haina nguvu.
“Madai ya kwamba
Tanesco inaidai IPTL Sh321 bilioni msingi wake ni dhana kwamba mtaji wa
IPTL ni Dola za Marekani 100, sawa na Sh50,000 kwa wakati huo. Dhana hii
ilipuuza ukweli kwamba Dola za Marekani 38.16 milioni ziliwekezwa
kwenye mradi wa Tegeta,” alisema.
Profesa Muhongo alisema
Bodi ya Tanesco imekana kuyatambua madai hayo ya Sh321 bilioni...
“Kimsingi hata vitabu vya hesabu vya Tanesco ambavyo vimekuwa
vikikaguliwa na CAG, havionyeshi kuwapo kwa deni hilo.”

11:23 AM
SAKATA LA ESCROW ASKOFU KILAINI NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA
Baba
Askofu Methodius KilainiDar es Salaam. Askofu Msaidizi wa Jimbo la
Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa
Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa
kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi
huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.
Askofu
huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa
viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika
akaunti ya escrow.
Katika
ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa
fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni
Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye
Simon (Sh40.4 milioni).
Akizungumza
kwa simu jana, Askofu Kilaini alisema Rugemalira hupendelea kuchangia
kwa uwazi miradi ya kijamii na si yeye peke yake aliyempatia mchango,
bali kuna watu wengine wengi ambao wameshampatia na kazi yake ni
kuipokea na kuifikisha sehemu husika.
Hata hivyo, kabla hajafafanua zaidi hoja yake, simu ilikatika na baadaye hakupatikana tena.
Hata
hivyo, jana askofu huyo alinukuliwa na Gazeti la Mawio toleo la jana
akisema fedha alizozipokea kutoka kwa Rugemalira ni kwa ajili ya miradi
mbalimbali inayoendeshwa na Kanisa Katoliki.
“Ndiyo
nimepokea fedha kutoka kwa James na hii siyo mara ya kwanza, kwani mara
nyingi amekuwa akichangia miradi mbalimbali ya kijamii,” alisema Askofu
Kilaini.
Alipotakiwa
na gazeti hilo kuwataja wengine waliochangia kanisa lake na kama nao
wamechanga kutoka kwenye fedha za akaunti ya escrow, alisema yeye hayumo
kwenye michango hiyo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
0 comments: