Na. Vero Ignatus Arusha
Waziri wa Habari ,Mawasiliano Teknolojia ya habari Jerry Slaa, amefungua kongamano wa siku mbili (Connect2Connect Summit)ambapo umewakutanisha wadau wote wa Mawasiliano nchini pamoja na wadau wengine ambapo amesema Watanzania zaidi ya Mil.75 wana simu za mkononi 35% wanamtandao wa intaneti ambapo mwaka mei 2023 Serikali ilizindua mkakati wa ujenzi wa minara 758 kupitia USAF mfuko uliotengenezwa na serikali ambapo kila mtoa huduma anachangia ili kupeleke huduma
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mhe. Always alisema minara mingine 636 mradi huo utaanza Oktoba 2024 huku akiwataka wananchi wanaofanya shughuli zao kupitia mitandao wapo salama zaidi na Serikali imetunga Sheria ya kulinda data za mtu binafsi katika matumizi ya mtandao na kila mtumiaji analindwa na hairuhusiwi kutumia data za mtu bila ridhaa yake.
Aidha Waziri Slaa,amesema hadi sasa 89% ya Watanzania wanapata huduma mtandao lengo likiwa Wananchi wote wapate huduma ya mtandao wa Internet,simu ,habari ,redio na televisioni yakuwemo maeneo ya Utalii ambayo yamepewa kipaumbele
Joseph Muhere, ni Mkurugenzi wa biashara Kampuni ya smu za mkononi,Airtel , amesema mwaka 2013 kampuni hiyo ilifunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa wenye uwezo wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani kwajili ya mawasiliano.
"Airtel mwaka huu 2024 inaendelea kufangua huduma zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini kuwezesha kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G"Amesema .
Muhere,alifafanua kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo sasa wanajenga huduma ya 5G kwa ajili ya wateja Ujenzi ambao unaenda sambamba na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu.
Kwa upande wake injinia Cecil Mkomola Francis mkurugenzi wa ufundi na Uendeshaji wa Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL amesema wanadhamana kubwa ya kutoa huduma ya mawasiliano, kupitia mkongo wa mawasiliano wa Taifa kwani wameendelea kufanya kazi na kuhakikisha kuwa nchi inaongea kwa kuunganishwa mikoa wilaya ambapo jumla ya wilaya 106 zimeunganishwa Tanzanzania bara Kati ya wilaya 139,mkongo huo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano na Intaneti.
Amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo kama Shirika ni kutoa mchango mkubwa wa mawasiliano kuhakikisha kwamba wanafikisha huduma kwa Wananchi na kupungiza gharama za matumizi.
0 comments: