Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu akikagua eneo lililowekwa mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni wakati akizundua mtambo huo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116
Mhandisi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abella Rwiguza akimuelezea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu namna mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni unavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa mtambo huo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116 |
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akitoa taarifa ya namna mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni unavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa mtambo huo uliofanywa leo na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu jijini Dar es Salaam. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) baada ya kuzundua mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni leo katika Hospitali ya JKCI Dar Group iliyopo jijini Dar es Salaam. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu baada ya kuzundua mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni leo katika Hospitali ya JKCI Dar Group. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116
Picha na: KHAMISI MUSSA
*********************************************************************************************************************
Mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni uliogharimu milioni 526,604,116 umezinduliwa leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group.
Mtambo huo uliozinduliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu umenunuliwa nchini Uturiki kwa shilingi milioni 320 na kugharimu milioni 70 kwaajilii ya kasha lakuhifadhia mtambo huo na usafirishaji, na milioni 136,604,116 zilitumika kwaajili ya kusimika mtambo huo tayari kwa kusambaza hewa ya oksijeni katika wodi za JKCI Dar Group na sehemu zingine.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati akizindua mtambo huo Mhe. Zungu alisema mtambo huo umefadhiliwa na Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) ikiwa ni sehemu ya kurejesha baadhi ya mapato yao kwa wananchi wenye uhitaji wa oksijeni.
Mhe. Zungu alisema kutokana na mtambo huo kuwa sehemu ya TBA kurudisha katika jamii, hivyo hivo JKCI iwe sehemu ya kutumia mtambo huo na kuwawezesha wananchi kupata huduma nafuu, safi, salama na kupunguza makali ya gharama za huduma za matibabu.
“Nawaomba Taasisi ya Moyo baada ya kuanza kutumia oksijeni mtakayozalisha katika mtambo huu gharama ziwe nafuu ili kuwawezesha wagonjwa wanaohitaji oksijeni kuipata kirahisi”, alisema Mhe. Zungu
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo alisema mtambo huo unatumia umeme wa KVA 60 na kuzalisha hewa ya oksijeni yenye ujazo wa milimita skweya 21 kwa saa yenye kasi ya mita skweya 5 kwa saa wakati wakujaza kwenye mitungi.
“Mtambo huu una vifaa vingi ikiwemo kifaa cha kupima ubora wa oksijeni inayozalishwa, kifaa cha kusafirisha oksijeni, kifaa cha kujaza hewa, kifaa cha kukausha hewa hadi kufikia skweya mita 312 kwa saa”, alisema Dkt. Delilah
Dkt. Delilah alisema mtambo huo una tanki la kupokea hewa lenye ujazo wa lita 1000 na tanki la kupokea hewa ya oksijeni wakati wa kutoa lenye ujazo wa lita 1000 hivyo ni jukumu la wafanyakazi wa JKCI kuulinda ili uweze kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa wanaohitaji huduma za oksijeni.
Dkt. Delilah alisema mtambo huo utapunguza gharama za uendeshaji kwa asilimia zaidi ya 3.7 kwa mwaka hivyo kuleta urahisi wa utoaji wa huduma ya haraka kwa wagonjwa na uzalishaji utakavyoongezeka huduma ya kusambaza oksijeni itatolewa katika hospitali zinazowazunguka.
“Kutokana na umuhimu wa hewa ya oksijeni katika hospitali na vituo vya afya kwa wagonjwa wanaohitaji kuongezewa hewa ya oksijeni JKCI Dar Group ilikuwa ikinunua oksijeni kwa kujaza mitungi kutoka kwa watoa huduma mbalimbali kwa gharama kubwa”, alisema Dkt. Delilah
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mabenki Tanzania (TBA) Herman Kasekende aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada inayofanya kuboresha huduma za afya nchini.
Herman alisema kila mwananchi anatamani kuwa na afya bora, umoja wa mabenki Tanzania unaendelea kuwezesha katika jitihada na mipango inayofanywa na Serikali pamoja na wadau wengine kuhakikisha wanajenga Tanzania yenye afya bora.
“TBA tumeweza kusimika mtambo wa kuzalisha oksijeni katika Taasisi hii ikiwa ni sehemu ya umoja wa mabenki Tanzania kuirudishia jamii kile tunachopata ili jamii nayo iweze kufaidia kupitia umoja huu”, alisema Herman
Herman alisema watu wanaweza wasione umuhimu wa kuwekeza mtambo huo kwasababu hawana uhitaji wa oksijeni kwa sasa lakini siku wakiwa na uhitaji ndio wataelewa thamani ya uwekezaji uliofanywa na umoja wa mabenki Tanzania.
0 comments: