MHESHIMIWA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AMWAGA AJIRA MPYA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:47 PM Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa ajira kwa Watumishi 21,200 katika kada ya ualimu 13,130 na Afya 8,070 kwa niaba ya Vijana wa Mkoa wa Singida tunamushukuru Mheshimiwa Rais kwa Upendo huu kwa Vijana.
Nina mambo kadhaa ya kuwakumbusha waombaji
Hakikisha unaomba mwenyewe au unasimamia kukamilika kwa maombi kwa mtu anayekusaidia,Kuna waombaji wanamwambia mtu akusaidie na anakuwa na nyaraka za waombaji wengi hivyo wakati wa kuambatanisha vyeti anachanganya cha Mwajuma anaweka kwa Sungura,Maombi hayo hayawezi pokelewa maana Vyeti vinakuwa pungufu au vimechanganywa.
CV ziandikwe vizuri na ziwe current na wadhamini ni watu wa karibu wanaokufahamu anaweza kuwa Mwalimu Mkuu wa Shule unakojitolea.
Andika Barua official na siyo Barua ya kirafiki,Huwezi Amini Kuna Watu wahajuwi kuandika barua Rasmi,Sasa hii ni Changamoto unaweza andika then ukapeleka kwa watu kadhaa wakaona ulivyo andika ili Barua yako iwe vizuri na inayoeleweka
Zingia muda wa Kutuma Maombi Kuna Watu huwa wanasubiri Siku za Mwisho,muda upo fanya maombi ndani ya Muda uliotajwa.
Amini kuwa Kwa msaada wa Mungu utafanikiwa Acha kutanguliza Rushwa na ukikosa Amini ipo Siku utapata Mheshimiwa Rais anajuwa Changamoto ya Vijana Nchini usipo pata leo utapata Kesho.
Na
Afisa Vijana Mkoa wa Singida.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: