Akizungumza katika ziara yake kwenye eneo la Tendegulu mkoani Lindi, aneo ambalo mabaki ya mjusi mkubwa anayefahamika kama Dinosaria yalipatikana mwaka 1908, anasema kama nchi haikuwa imeendelea wakati huo na waliweza kuvumbua mabaki, basi ni wakati wa nchi kuwekeza nguvu kubwa kwenye tafiti ili waweze kugundua mabaki mengine zaidi kwani anaamini mjusi mkubwa aliye nchini Ujerumani kwenye makumbusho lazima atakuwa na wenzake ambao bado hawajaonekana nchini.
Aidha, kutokana na kuwepo kwa mali kale adhimu katika eneo hilo la Mipingo, Dr Kikwete ameahidi rasmi kuwepo kwa ujenzi wa makumbusho ya Taifa ili taarifa na mabaki ya kale yatakayopatikana katika eneo hilo viweze kutunzwa na kuhamasisha utalii kwani eneo hilo ndipo anapotoka mjusi mkubwa duniani ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Ujerumani
0 comments: