

Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) akiongea na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi.
Wang Ke (Kulia) katika ofisi za Wizara Mkoani Dodoma.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke
(Kulia) wakiweka saini makubaliano ya kukabidhiana vifaa vya ofisi
vyenye thamani ya shilingi milioni 133 katika ofisi za Wizara Mkoani Dodoma.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa
China nchini Bibi. Wang Ke (wa pili kulia) pamoja na watendaji wa Wizara Mkoani Dodoma. (Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,DODOMA)
Na Lorietha Laurence-WHUSM,Dodoma
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
amemshukuru Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke kwa
kuipatia wizara vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 133.
Waziri
Dkt. Mwakyembe ametoa shukrani hiyo leo Ofisini kwake Mkoani Dodoma
alipokutana na Balozi huyo ambapo waliweka sahihi ya makabidhiano ya
vifaa hivyo na kuhaidi kuendelea kuimarisha uhusiano huo uliodumu kwa
muda mrefu .
“Nashukuru
sana Balozi kwa kutupatia msaada wa vitendea kazi na tunaahidi
kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya nchi hizi mbili kwa manufaa ya
taifa na watu wake” amesema Mhe.Dkt. Mwakyembe.
Aidha
Waziri Dkt. Mwakyembe ameongeza kuwa tayari kumekuwa na juhudi za wazi
zinafofanywa na Ubalozi huo kwa kutoa mafunzo ya kubadilishana utaalam
kati ya Tanzania na Jamhuri ya watu wa china kupitia sekta za filamu,
habari,michezo na utamaduni.
Pia,
Dkt. Mwakyembe alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania imepata nafasi ya
kuwa Mwenyekiti wa programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika
wenye lengo ya kuhifadhi kumbukumbu za harakati za kuikomboa Afrika ili
kuwa na historia nzuri kwa kizazi kijacho.
“Tayari
tumeanza maandalizi ya kuhifadhi historia ya wapigania uhuru
ukizingatia Tanzania ilikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha nchi za
Bara la Afrika zinakuwa huru, hii ni hatua kubwa kwetu katika kuimarisha
mahusiano baina ya nchi zetu ” amesema Mhe. Dkt. Mwakyembe.
Naye
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini Bibi. Wang Ke ameeleza
kufurahishwa na ushirikiano ulipo baina ya nchi hizo mbili ikiwemo
kujifunza tamaduni za China.
“Nimefurahi
kuona idadi kubwa ya watanzania wanaojifunza utamaduni wetu kupitia
Chuo kikuu cha Dar es Salaama na Chuo kikuu cha Dodoma, ni hatua nzuri
na ya msingi katika kuimarisha mahusiano ya nchi zetu” amesema Balozi
Wang Ke.
Tanzania
na Jamhuri ya Watu wa China wamekuwa na ushirikiano wa karibu katika
kuleta maendeleo tangu mwaka 1960 ambapo walishirikiana katika ujenzi wa
reli ya TAZARA na sasa uhusiano huo umezidi kuimarishwa kupitia sekta
za habari,filamu, sanaa na utamaduni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: