Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Watu wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi wa masuala ya Ukimwi kwa wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia masuala ya UKIMWI wakati wa warsha
ya wajumbe wa kamati hiyo iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba 14, 2017.
Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Taifa ya kudhibiti
Ukimwi Dr. Leonard Maboko akichangia hoja kuhusu masuala ya Ukimwi wakati wa Warsha
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI iliyofanyika Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala
ya UKIMWI Mhe. Daniel Mtuka akifafanua jambo wakati wa warsha kwa wajumbe wa
kamati hiyo kuhusu masuala ya Ukimwi nchini iliyofanyika Bungeni Dodoma Novemba
14, 2017.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Masuala ya UKIMWI Mhe. Martha Mlata akichangia hoja wakati wa warsha
iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi kuhusu masuala ya Ukimwi iliyofanyika
Mjini Dodoma.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Masuala ya UKIMWI Mhe.Zainab Bullu akifafanua jambo wakati wa warsha kwa
wajumbe wa kamati hiyo iliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya kudhibiti Ukimwi.
Na
MWANDISHI WETU
Ofisi
ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Taifa yakudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imedhamiria
kuendelea kuwajengea Uwezo Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia
Ukimwi ili iweze kushiriki vyema katika mapambano dhidi ya Ukimwi.
Akizungumza
wakati wa Semina ya siku tatu iliyoanza leo mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista
Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa vita dhidi ya
janga la Ukimwi inafanikiwa ili kulinda nguvu kazi ya Taifa.
“Serikali
imejipanga kuhakikisha swala hili linapewa kipaumbele hasa katika kutoa elimu
kwa wananchi ili waweze kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya
UKIMWI” Alisisistiza Mhe. Mhagama
Akifafanua
Mhe. Mhagama amesema kuwa vita dhidi ya janga la Ukimwi niya kila Mtanzania
hivyo ni vyema wadau wote wakashirikiana na Serikali katika mapambano hayo.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi Mhe.
Daniel Mtuka amesema Warsha hiyo
inajenga msingi kwa wajumbe wa Kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
Aliongeza
kuwa Wajumbe wa Kamati hiyo wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kupambana
na Ukimwi hapa nchini ili kuhakikisha kuwa
malengo yakuondoa janga hilo hapa nchini yanatimizwa kwa wakati muafaka.
Kwa
Upande wake mmoja wa wajumbe wa Kamati hiyo Mhe. Martha Mlata amesema kuwa ni
wakati muafaka sasa kwa jamii kushiriki kikamilifu katika vita dhidi ya Janga
la Ukimwi kwa kusimamia maadili katika Jamii hali itakayochochea kuleta
mabadiliko.
Warsha
ya Siku tatu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inashughulikia Ukimwi
inafanyika mjini Dodoma kwa siku tatu ikilenga kuwajengea uwezo wajumbe wa
Kamati hiyo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha.
0 comments: