ALIYEKUWA MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE ATOA MSAADA WA ZAIDI YA MIL. 11. 7 KWA WATOTO WENYE MAHITAHI MAALUMU

 Baadhi ya msaada mbalimbali
Mtemvu akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Juni 18, 2017, wakati alipokuwa akitowa msaada kwa vikundi vya watu wenye mahitaji maalumu na kwa vikundi vya watoto yatima, zaidi ya vikundi 8 vimefanikiwa kupata msaada huo, aliendelea kusema 


Japo nilikuwa safarini, Oman lakini nikawahi kuja kumzika mama yangu kipenzi na ikanichukuwa kulianza zoezi hili kutoka na  wageni ambapo kawaida yangu huanza mwanzoni mwa mwezi  Mtukufu wa Ramadhani. alisema Mtemvu

Naomba mnisamehe kwani kawaida huanza katika kumi la mwanzo
lakini kutokana na msiba huo na kuwa na wageni ndio maana tumechelewa, napenda kutowa shukurani zangu za dhati kwa wana Temeke na wana Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla, Alisema,  Mtemvu,

Niahadi yangu niliyoiahidi katika maisha yangu ahadi hii ninaitimiza na kwa kusaidia jamii kwani nikijaaliwa nitakuwa nayafanya haya na pia watakao hitaji kwenda kuhiji Makka ninazo nafasi kwa watakao hitaji nikufanya mawasiliano nitawapeleka 

Namuomba Mungu anipe uhai  nizidi kuwahudumia, na kuna
vikumdi vitatu ambavyo havikufika na kushauriana na mama wa vituo vitatu kimojawapo ni kikundi cha makao tunaomba siku ya Idd tutawapelekea
 Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza na watoto na walezi wenye mahitaji maalumu Dae es Salaam leo Juni 18, 2017. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kulia) akimkabidhi Afisa Ustawi wa Jamii, Jack Omary (wa pili kushoto) msaada wa unga wa ngano ikiwa ni moja ya msaada wa mafuta ya kula, sukari, unga wa sembe, kwa ajili ya kituo cha Taifa cha kulelea watoto wenye shida maalumu cha Kurasini chenye watoto 72, kulia ni  Khalid Saidi Darasa la Tano Shule ya Mtoni Sabasaba Dar es Salaam, kushoto ni Zuwena Dotto na watatu kulia ni mama Mtemvu




0 comments: