Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mtanzania ,Anna Makinda
amewataka wanawake wa bara la Afrika kusimama imara ili waweze kuwa
viongozi makini katika kupambana siasa kandamizi kwa Wanawake katika
bara la Afrika.
Makinda
amesema kuwa zaidi ya miongo kumi imetajwa kuwa huenda mwanamke wa
kiafrika akapata ukombozi katika siasa za bara hili,ambazo zinatazamwa
kuwa na mlengo wa mfumo dume tangu kuondoka kwa wakoloni .
Aidha
hayo yamebainishwa katika mjadala wa kigoda cha Mwalimu unaofanyika kila
mwaka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali,na kuongeza kuwa siasa za
Africa bado zinawagawa wanawake katika mlengo wa kisiasa na kijamii.
"harakati
na mambo mengi yamefanyika ili kumkomboa mwananmke wa Afrika na mfumo
dume,lakini yote haya yanaonekana kutofanikiwa kwa asilimia miamoja na
changamoto ikionekana kuwapo kwa wanawake wenyewe kwa
kutothaminiana"amesema Makinda.
Anna
makinda amekuwa kiongozi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa serikali ya awamu iliopita, anatazama changamoto hii kwa wasichana
wa sasa kuwa ni kubwa sana kutokana na mazingira yanayowazunguka .
Spika wa Bunge Mstaafu, Anna Makinda akizungumza katika mkutano wa
Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, ambapo mada ya
Nafasi ya Wanawake na Siasa za vyama vingi katika bara la afrika
iliwasilishwa na wanawake mbalimbali viongozi.
Mbunge wa Jimbo la Hanang,Mary Nagu akizungumza wakati wa
kongamano la Kigoda cha Mwalimu Nyerere Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
ambapo mada ya nafasi ya Wanawake katika uongozi bara la afrika
iliwasilishwa.
Mbunge wa Bunge la Uganda Miria Matembe, akizungumza wakati wa
Kigoda cha Mwalimu juu ya nafasi ya Wanawake katika Siasa za Afrika
Sehemu ya Washiriki waliofika kusikiliza kigoda Cha Mwalimu juu ya nafsi ya Mwanamke katika Siasa za bara la Afrika
Muongozaji wa Mdhalo wa Kigoda cha Mwalimu juu y Mada ya Nafasi ya
Wanawake katika siasa za bara la Afrika,Mary Rusimbi akizungumza katika
kongamano hilo.
Sehemu ya Washiriki wa Kigoda cha Mwalimu katika ukumbi wa Nkurumah chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Mwanafunzi wa kitivo Cha Sheria Chuo kikuu cha Dar es Salaam,Edda Gideon akichangia mada katika kongamano la kigoda cha mwalimu
Mmoja wa washiriki akichangia mada katika kigoda hicho cha Mwalimu Nyerere
Mwanasiasa Mkongwe , Anna Abdalah akichangia mada katika kongamano
la Kigoda cha Mwalimu Nyerere juu ya nafasi ya wanawake katika Siasa za
bara la Afrika
Profesa ,Ruth Meena akichangia jambo katika Kigoda cha Mwalimu juu ya mada ya nafasi ya Wanawake katika siasa za bara la Afrika.
Mwenyekiti wa Tasisi ya Jinsia katika kigoda cha Mwalimu Nyerere,
Dk Eugenia Kafanabo akiongea wakati wa kufunga mjadala wa kigoda cha
Mwalimu
Viongozi wa Meza kuu katika mjadala wakiwa katika picha ya Pamoja
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: