WANAJESHI WA YEMEN WALIPIZA KISASI KWA KUUA ASKARI 13 WA SAUDIA

Wanajeshi wa Yemen wametekeleza oparesheni kubwa ya kulipiza kisasi na kuuawa wanajeshi 13 Wasaudi katika maeneo kadhaa ya kusini magharibi mwa Saudi Arabia.
Askari sita kati ya waliouawa walikuwa katika kituo cha kijeshi cha Al Fuaz katika eneo la Najran nchini Saudi Arabia.
Wanajeshi wa Yemen pia wameshambulia gari la deraya na kuangamiza askari watatu Wasaudi waliokuwa katika kituo cha kijeshi cha Alib eneo la Asir. Wanajeshi wengine wanne Wasaudi waliuawa katika eneo lililo karibu na hilo. Askari wa Jeshi la Yemen wakishirikiana na wapiganaji wa Ansarullah wamekuwa wakiilinda nchi hiyo ambayo ilivamiwa na Saudi Arabia Machi 2015.
Wapiganaji wa Ansarullah
Saudia iliivamia Yemen kwa himya ya Marekani kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh.
Raia zaidi ya elfu 12  wa Yemen wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. 

0 comments: