RAIS MAGUFULI ASHINDWA KUJIZUIA ,ATOKWA NA MACHOZI,SOMAHAPO KUJUA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ametoa neno na kusema amepatwa na uchungu na majonzi baada ya kuona majeneza ya watoto na walezi wao ambao walipata ajali ya basi huko Arusha.

Rais Magufuli amesema hayo kupitia ukurasa wake wa twitter na kuwataka Watanzania kuomboleza msiba huu kwa umoja huku tukiwaombea marehemu hao wapumzike mahali pema peponi.

"Nimepatwa na uchungu na majonzi makubwa ninapoyaona majeneza ya watoto na walezi wao waliopoteza maisha katika ajali ya basi huko Arusha, tumewapoteza mashujaa wetu katika elimu. Tuwaombee na tuendelee kuwa na subira, uvumilivu na ustahimilivu, tunapoomboleza vifo vya wapendwa wetu tuendelee kuwa wamoja. Mungu ibariki Tanzania" alisema Rais Magufuli 

Mbali na hilo miili yote ya marehemu ambayo imeagwa leo katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha imesafirishwa na kuelekea sehemu mbalimbali za nchi kwa ajili ya ndugu kufanya maziko ya wapendwa wao hao

0 comments: