Historia
wakati mwingine huwa ina umuhimu sana katika maisha ya soka, usiku wa
Mei 3, 2017 katika uwanja wa unaotumiwa na AS Monaco kama uwanja wa nyumbani
Monaco waliikaribisha Juventus kucheza mchezo wao wa kwanza wa nusu
fainali ya pili ya UEFA Champions League msimu wa 2016/2017.
Mchezo wa
nusu fainali ya pili ya kati ya Juventus dhidi ya Monaco kivutio
kilikuwa ni golikipa wa Juventus Buffon na mshambuliaji wa Monaco Mbappe
ambaye ameonesha umahiri mkubwa katika michuano hiyo kwa siku za
karibuni, Mbappe amezaliwa mwaka 1998 alikuwa anajitahidi kumfunga
Buffon ambaye mwaka anaozaliwa Buffon alikuwa anacheza World Cup yake ya
kwanza.
Buffon
amefanikiwa kumdhibiti Mbappe ambaye ameonesha makali lakini Buffon pia
hajawahi kufungwa goli na Lionel Messi ambaye ni moja kati ya wachezaji
bora wa muda wote wa kizazi cha sasa, hata hivyo Juventus wamefanikiwa
kupata ushindi wa magoli 2-0 katika mchezo huo wa kwanza, magoli
yamefungwa na Gonzalo Higuan dakika ya 29 na 59.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: