WAZIRI MKUU MAJALIWA - WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:38 AM
Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali
yao na kuvipa muda vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya
matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyotokea nchini ili kubaini chanzo cha
matatizo na wahusika.
Aidha,
Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea na utamaduni wa
kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea
vitendo vya kihalifu au viashiria vyake katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri
Mkuu ametoa kauli hiyo leo, Aprili 20, 2017) Bungeni mjini
Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu
wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni,
Mheshimiwa Freeman Mbowe aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya hofu
iliyotawala nchini kuhusu vitendo vya watu kuuliwa, kupotea na kutekwa.
Waziri
mkuu amesema “tukitoa taarifa mapema tunaweza kuharibu upelelezi,
tuviachie vyombo vetu vya dola viendelee kufuatilia kuona nani
anayesababisha vitendo hivyo na dosari iko wapi na nini chanzo chake
alisisitiza,”.
Kadhalika
Waziri Mkuu amewasii Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu
kuheshimiana, kufuata kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza
majukumu yake. “Moja ya majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania
wanaishi kwa amani kwa kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali
zao wakati wote,”.
Hata
hivyo, Mheshimiwa Mbowe aliishauri Serikali kushirikiana na vyombo vya
kiuchunguzi vya kimataifa kuchunguza tukio la kupotea kwa msaidizi wake
Ben Saanane lililotokea miezi sita iliyopita, ambapo Waziri Mkuu amesema
kuwa Taifa lina mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali na inashirikiana
nayo katika mambo mbalimbali likiwemo suala ya ulinzi ambapo si rahisi
kuainisha namna wanavyoshirikiana.
Waziri
Mkuu ameongeza kuwa vyombo vyetu vina weledi,vifaa na uwezo wa kutosha
kufanya uchunguzi juu mambo yanayotokea nchini hivyo amesisitiza
wananchi kuendelea kuiamini kwani matukio haya ya kihalifu likiwemo la
mtu kutoweka au kufariki na haina kikomo cha uchunguzi, mara zote
uchunguzi unategemeana na aina ya tukio lenyewe au mazingira lilipo
tokea
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya mapitio kwa vyama
vyote vya Ushirika nchini kufuatia baadhi ya vyama hivyo kuwa na
mwenendo mbaya hali inayochangia upotevu wa fedha nyingi na kukatisha
tamaa wakulima.
Amesema
hivi karibuni katika kikao cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika
wilayani Bagamoyo Bodi ya Korosho ilidaiwa kuhusika na ubadhilifu wa sh.
bilioni 30 ambapo Serikali iliunda timu maalumu ya uchunguzi na kubaini
upotevu wa sh. bilioni sita na siyo sh. bilioni 30.
Hata
hivyo amesema kwamba hasara hiyo ya sh. bilioni sita haikusababishwa na
bodi bali vyama vikuu na vya ushirikika vilivyopo kwenye ngazi ya Kata
na wilaya, ambavyo vyote vilifanyiwa uchuguzi na hatua zimeanza
kuchukuliwa.
Amesema
matatizo hayo yako katika vyama vyote vya ushirika hususan vya mazao ya
Tumbaku, Kahawa,Pamba, Chai na mazao mengine makuu, ambapo Serikali
imeanza kupitia taarifa za ukaguzi kwa kina ili iweze kufanya ukaguzi na
sasa wanaendelea na uchunguzi wa chama kikuu cha tumbaku.
Waziri
Mkuu amesema wakimaliza kufanya uchunguzi katika chama kikuu cha
tumbaku watachunguza vyama vingine vya pamba, kahawa na chai lengo
likiwa ni kuwalinda wakulima na kuhakikisha wanapata tija. “Naomba
kusisitiza hatua zinaendelea kuchukuliwa na tutaendelea kuimarlisha na
ushirika,”.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mama Salma
Kikwete aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu
ubadhirifu wa sh. bilioni 30 uliofanywa na Bodi ya Korosho nchini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S.L.P 980, DODOMA
APRILI 20, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijibu maswali bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi
wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, (kulia) bungeni mjini Dodoma,
Aprili 20, 2017.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: