WALIOHUSIKA NA KUWADHALILISHA SHAKHSIA WA IRAQ WATACHUKULIWA HATUA KALI

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan amemuhakikishia Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq kwamba, watu waliohusika na kuwavunjia heshima shakhsia muhimu wa Iraq, wametiwa mbaroni na kwamba watafikiishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Ayman Safadi ameyasema hayo katika mazungumzo ya simu na waziri mwenzake wa Iraq, Ibrahim al-Jaafari ambapo sambamba na kusisitizia umuhimu wa kuimarishwa mahusiano baina ya Aman na Baghdad, amesema kuwa Jordan inalaani aina yoyote ya uvunjiwaji heshima taifa la Iraq.
Ahmad Jamal, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq
Kabla ya hapo Ahmad Jamal, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq alikosoa vikali kimya cha serikali ya Jordan juu ya kitendo cha baadhi ya raia wa nchi hiyo cha kuwavunjia heshima baadhi ya shakhsia muhimu wa Iraq ikiwemo kuichoma moto picha za maraajii wakubwa wa nchi hiyo. Alisema kuwa, kitendo hicho ndicho kiliifanya serikali ya Baghdad kumwita balozi mdogo wa Jordan nchini Iraq, kwenda kujieleza katika Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo.
Nouri al-Maliki, Makamu wa Rais wa Iraq.
Jumamosi iliyopita, mbunge mmoja wa Iraq alitangaza kuwa, kundi moja la raia wa Jordan liliivunjia heshima picha za maraajii wa kidini na shakhsia wengine wa kisiasa akiwemo Nouri al-Maliki, Makamu wa Rais wa Iraq.

0 comments: