WAISLAMU MAREKANI WAFANYA KONGAMANO KUBWA LA DINI TATU ZA MBINGUNI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 1:31 AM
Waislamu wa mji wa Baltimore, nchini Marekani
wamefanya kongamano la 42 la kila mwaka la Waislamu wa nchi hiyo kwa
kushiriki Waislamu elfu 20 kutoka maeneo mbalimbali ya taifa hilo.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya
Kiislamu ya (ICNA) nchini Marekani imetangaza kuwa, kongamano hilo la
siku tatu limejadili kadhia ya 'Juhudi kwa ajili ya Mafanikio ya kweli
na Ujumbe wa Mungu wa Musa, Issa na Nabii Muhammad (saw)' hapo
mjini Baltimore katika jimbo la Maryland, mashariki mwa Marekani.
Kadhalika ofisi ya Kiislalmu ya kaskazini mwa Marekani (ICNA)
imesisitiza kuwa, katika kongamano hilo kumefanyika pia vikao mbalimbali
na kujadili masuala kama vile, kukabiliana na chuki dhidi ya dini ya
Kiislamu, kutetea haki za Waislamu katika kipindi cha utawala wa Rais
Donald Trump, wa Marekani, ongezeko la jinai dhidi ya Waislamu na
hatua hasi ya serikali ya rais huyo ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini
humo.
Kadhalika Waislamu nchini Marekani wamepata kutoa malalamiko yao
kuhusiana na matatizo mbalimbali yanayowakabili ndani ya taifa hilo
hususan baada ya kuingia madarakani Rais Trump mwenye misimamo ya
kibaguzi na chuki. Wakati huo huo, zaidi ya watu 1000 wasio na makazi
walipatiwa misaada mbalimbali ikiwemo ya chakula, ambayo ilitolewa na
kundi la wafuasi wa dini tatu za Uyahudi, Ukristo kwa kushirikiana na
Waislamu wa Baltimore.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: