WACHEZAJI 2 MUHIMU MOURINHO ANAOWATAKA KUUNGANA NA ZLATAN! MAN UTD
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:25 PM
JOSE
MOURINHO anashawishika sana kumtaka Romelu Lukaku na Antoine Griezmann
ili kuweza kuongeza nguvu kwenye kikosi chake na wachezaji hao kuungana
Zlatan Ibrahimovic Manchester United.The Old Trafford boss ametenga
kiasi kikubwa cha pesa (Mtonyo) wa £160million kwaajili ya kuimarisha
kikosi chake na pia kumuacha kipenzi cha Manchester united Wayne Rooney
ambae anajiandaa kuondoka Klabuni hapo..Mourinho pia anataka kumfanya
Ibra kuwa godfather mpya wa Old Trafford kwa kumuongezea mkataba mpya
wa kumfanya mswedeni huyo kubaki OT kwa mwaka mwingine tena wenye
thamani ya £10m.The Special One kesho anaingia kwenye mchezo mgumu na
wa muhimu watakapokutana na Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani OT ili
kujiweka kwenye nafasi nzuri ya timu yake kurudi kwenye Champions
League..Wachezaji ambao Mourinho anawafukuzia kwa muda mrefu bila kukata
tama ni Antonie Griezmann wa Athletico Madrid, Dili la mchezaji huyo
litafanikiwa zaidi kama Manchester united wakifanikiwa kumaliza Top 4
kwenye Epl na kwenda Champions League..
Pia
mchezaji mwingine ambae Jose anamfukuzia ni Romelo lukaku ambae
alimpeleka West Brom kwa mkopo na baadae kwenda Everton wakati
anaifundisha Chelsea kabla ya kutua kwa mashetani wekundu..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: