MIILI YA ASKARI NANE WALIOUAWA MKOANI PWANI YAAGWA JIJINI DAR, WAZIRI MWIGULU ATANGAZA KIAMA KWA WATUHUMIWA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:25 PM
WAZIRI
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amewatangazia kiama watu
wote waliohusika kuwaua askari polisi nane Kibiti wilayani Mkuranga
mkoani Pwani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa heshima za mwisho
Dar es Salaam leo mbele ya majeneza yenye miili ya askari nane waliouawa
na majambazi Kibiti wilayani Mkuranga mkoani Pwani juzi jioni.Kulia
kwake ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamad Masauni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba, akitoa pole kwa wafiwa.
Ndugu,jamaa na marafiki wa wafiwa wakiwa katika shughuli hiyo ya kuaga miili ya wapendwa wao.
Maofisa wa Uhamiaji wakiwa kwenye shughuli hiyo.
Wananchi wakiwa katika shughuli hiyo ya uagaji wa miili hiyo.
Maofisa wa Polisi wakishiriki kuaga miili ya wenzao hao.
Foleni ya kuaga miili hiyo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchini, Mwigulu Nchemba (kulia), akiteta jambo na
Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu wakati wa kuaga miili hiyo.
Mmoja wa ndugu za askari hao akilia kwa uchungu.
Ni kilio kwa kuwapoteza wapendwa wao.
Ni huzuni.
Na Dotto Mwaibale
Akizungumza
wakati wa kuaga miili ya askari hao jijini Dar es Salaam leo asubuhi
Mwigulu alisema watu hao watakamatwa wote na kufikishwa kwenye mkono wa
sheria. "Kitendo hiki cha mauaji kilichofanyika dhidi ya askari wetu
hakivumiliki hata kidogo waliohusika tutawatafuta na kuwakamata" alisema
Mwigulu.
Aliwaomba
wananchi wa maeneo husika kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili
kuwapata wahusika wa tukio hilo. Katika hatua nyingine Mwigulu ameitaka
wizara husika kuhakikisha inatoa fidia kwa ndugu wa askari hao na
majeruhi badala ya kuchukua muda mrefu kuitoa. "Naomba fidia kwa askari
hawa tuliowapoteza wakitumikia taifa itolewa haraka bila kucheleweshwa"
aliongeza Mwigulu.
Mkuu
wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu alisema watuhumiwa wote
waliohusika kufanya mauaji hayo ni lazima watafikiwa na mkono wa dola.
Alisema wananchi wa eneo hilo wanawafahamu wahusika hivyo amewaomba
washirikiane na polisi ili kuwapata vinginevyo nguvu itatumika.
Alisema
linapotokea tukio kama hilo kuna baadhi ya watu wamekuwa wakishabikia
kupitia mitandao ya kijamii hivyo akatoa onyo kuwa watakao bainika na
wao watakamatwa kwa kutenda kosa.
Askari
waliopoteza maisha katika tukio hilo la kinyama wametajwa kuwa ni
pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC
Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: