Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wajumbe wa kamati za Siasa Tawi , wilaya na mkoa kwenye ukumbi wa TC Dunga, wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
Kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe 590 uliofanyika kwenye ukumbi wa TC Dunga , Mhe. Samia aliwataka wana CCM kukiimarisha chama katika mkoa wa Kusini Unguja , aliwaambia wajumbe hao kuwa CCMsi kadi CCM ni Itikadi, ambapo aliahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha mafunzo ya itikadi mara baada ya chaguzi ndani ya chama kukamilika.
Alihimiza Vijana waambiwe mambo mazuri ya CCM alisema "CCM peke yake, ndio penye misingi,penye historia, na penye Malengo" na kutaka wananchi hao kuunga mkono juhudi na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein katika kuleta maendeleo nchini.
Mhe. Samia pia alihimiza Makatibu kufanya kazi zao hasa katika kutoa taarifa sahihi za masuala ya uchaguzi badala ya kubeba watu na alizitaka Jumuiya kufanya kazi zake kwa mujibu wa kanuni na utaratibu.
Aidha wakati wa kumkaribisha Mhe. Samia , Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Dkt. Abdalla Juma Mabodi alisema Wazanzibar wapuuze porojo za wanasiasa waliopoteza muelekea kwani hata Jumuiya za Kimataifa zinaelewa CCM ndio inayotawala kwa mujibu wa Sheria na Katiba na aliahidi kufanya kazi zaidi na mashina.
0 comments: