Jaribio jipya la kufyatua
kombora Korea kaskazini limeshindwa
wakati liliporipuka baada ya kufyatuliwa Jumapili(16.04.2017)
siku moja baada ya nchi hiyo kuonesha hazina yake ya makombora
katika gwaride kubwa la kijeshi.
Makombora ya Korea kaskazini katika maonesha ya gwaride
Kushindwa huko , ambako kunaonekana kwa umma kama kitu cha
fadhaa kwa serikali ya nchi hiyo, kumekuja huku hali ya wasi
wasi ikiongezeka katika kanda hiyo kuhusiana na dhamira ya
Korea kaskazini kujipatia silaha za kinyuklia.
"kombora
hilo liliripuka mara moja," wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema
kuhusiana na jaribio hilo lililofanywa mapema leo asubuhi ambalo
taarifa zake zilipatikana kupitia jeshi la Korea kusini. Hata
hivyo haikuwezekana kufahamu mara moja ni aina gani ya kombora
lilitumika katika jaribio hilo, muda ambao unaonekana kuwa
uliamuliwa kwa makusudi kabisa.
Kombora la Korea kaskazini likifyatuliwa
Jaribio
hilo limekuwa baada ya Korea kaskazini kuonesha karibu
makombora 60 , ikiwa ni pamoja na kile kinachoshukiwa kuwa
kombora jipya linaloweza kuvuka mabara , katika gwaride siku ya
Jumamosi kuadhimisha miaka 105 ya kuzaliwa kwa muasisi wa taifa
hilo Kim II-Sung.
Sherehe hizo zilifanyika mbele ya kamera
za mashirika ya habari duniani yaliyoalikwa, ambayo yalikuwapo
pia Pyongyang wakati wa jaribio la kurusha kombora hilo
lililoshindwa. Kushindwa kwa kombora hilo kurushwa kunakuja masaa
machache kabla ya ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Mike
Pence nchini Korea Kusini ambako mpango wa silaha wa taifa
hilo lililoko upande wa kaskazini utakuwa ajenda ya juu.
Sherehe za kuadhimisha mwaka wa 105 wa kuzaliwa muasisi wa taifa la Korea kaskazini
Tabia ya ukaidi
Korea
Kaskazini ina tabia ya kurusha makombora kuadhimisha sherehe
muhimu za kisiasa, ama kama ishara ya ukaidi mnamo wakati
maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani wanapofanya ziara katika
eneo hilo.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis
amesema Trump amefahamishwa kuhusu jaribio hilo la hivi karibuni
lakini "hakutoa maelezo zaidi".
Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis
Tukio
la leo Jumapili la kurushwa kwa kombora kumefanyika majira ya
alfajiri kutoka Sinpo , eneo la kurushia makombora upande wa
pwani ya mashariki ya Korea kaskazini ambako nchi hiyo ina eneo
la kuegesha meli.
Mwezi Agosti mwaka jana, kombora
lililorushwa kutoka katika nyambizi kutoka Sinpo liliruka kilometa
500 kuelekea Japan. Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-Un
amesifu jaribio hilo kuwa "ni mafanikio makubwa" na kusema
limeiweka Marekani kuwa karibu na mfumo wa kurusha makombora
unaoweza kuhamishika.
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-Un
Trump hajasema lolote
Rais
Trump amesema mara kadhaa atazuwia Pyongyang kufikia lengo lake
la kutengeneza makombora yenye silaha za nyuklia yanayoweza
kufika nchini Marekani.
Huku uvumi ukiongezeka kuwa Korea
kaskazini inajitayarisha kufanya jaribio la sita la makombora ya
nyuklia ametuma meli ya kivita yenye ndege za kivita katika
rasi ya Korea--ishara ya wazi baada ya Marekani kufanya
shambulio la makombora nchini Syria.
Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: