Balozi wa Korea Kaskazini ameituhumu Marekani kuhujumu amani na
utengamano katika Rasi ya Korea wakati mvutano ukishamiri katika eneo
hilo. Akizungumza katika Umoja wa Mataifa Balozi Kim In-ryong
alisisitiza kuwa Korea Kaskazini iko tayari kwa vita kamili na Marekani.
Alisema mwenendo wa Marekani wa kutumia ubabe kuzivamia nchi huru na
baadaye kudai inachangia katika kulinda amani ya dunia ni kukosa
uwajibikaji. Korea Kaskazini ambayo hujulikana pia kama Jamhuri wa
Kidemokrasia ya Watu wa Korea ilizidisha mvutano wa kikanda kwa kufanya
jaribio jingine la kurusha kombora ambalo lilishindwa Jumapili.
Wanadiplomasia kadhaa wa nchi hiyo wamesema nchi yao itaendelea kufanya
majaribio mengine kila wiki, kila mwezi na kila mwaka.
KOREA KASKAZINI YALAANI MAREKANI KWA 'KUHUJUMU ' AMANI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:27 AM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: