Wagombea watakaozusha ghasia kwenye mchujo wa chama cha
Jubilee hawataruhusiwa kuwania viti mbalimbali chamani. Rais Uhuru
Kenyatta amesema pia sheria itazingatiwa bila upendelea kwa mtu yeyote.
Ujumbe wa Rais Uhuru Kenyatta unajiri siku nne kabla ya zoezi la
mchujo wa chama chake cha Jubilee kuanza. Zoezi hilo lilikuwa
linastahili kuanza siku ya Ijumaa lakini likaahirishwa na hapajatolewa
sababu za hatua hiyo. Akionekana mwenye ghadhabu, Rais Kenyatta
alisisitiza kuwa hakuna wawaniaji ambao wameteuliwa ama kupendekezwa na
chama chake. Aliwahakikishia wananchi kuwa wao ndio wenye uwezo wa
kuchagua viongozi wao. Rais alikuwa na onyo kwa wanachama ambao wana nia
ya kuzusha ghasia kwenye mchujo huo na wakati wa uchaguzi mkuu Agosti
tarehe nane.
Ghasia
na madai ya wizi wa kura kwenye mchujo wala hayajakisaza chama cha
upinzani cha ODM. Zoezi la mchujo wa chama cha ODM ulioanza juma
lililopita, umesababisha baadhi ya wanachama kuhamia vyama vingine kwa
madai ya kubaguliwa.
Huku
joto la kisiasa likizidi kuongezeka nchini, Muungano wa Upinzani NASA
hatimaye umeondoa taharuki kwa wafuasi wake kwa kutangaza kwamba mgombea
wa kiti cha urais kwa tikiti ya muungano atatajwa kwenye mkutano mkubwa
wa siasa tarehe 27 Aprili. Kwenye Mkutano uliotumiwa kumkaribisha
kiongozi wa chama cha Mashinani Gavana wa Bomet Isaac Ruto kuwa kinara
mwenza wa muungano wa NASA viongozi wa upinzani wameitaja siku ya leo
kuwa siku ya kihistoria katika siasa za Kenya.
Muungano
wa upinzani umezindua mkakati wake wa kushinda uchaguzi mkuu ujao
kwenye hafla hafla ya leo. Kalonzo Musyoka ni mmoja wa vinara
anayetarajia kutajwa kupeperusha bendera ya NASA
Viongozi hao
wameutaja muungano wa NASA kuwa muungano wa Wakenya wote. Muungano wa
NASA sasa unajumuisha vyama vitano vya ODM, Wiper Democratic Movement,
Ford Kenya, Amani National Congress na Chama cha Mashinani.
Viongozi wa Muungano wa upinzani NASA: Musalia Mudavadi, Raila Odinga, Isaac Ruto, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula
Siku
109 zimesalia uchaguzi mkuu kufanyika na uteuzi wa wagombea urais
unatakiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Mei. Kura za Mchujo za vyama
tanzu vya muungano wa NASA zilianza wiki iliyopita na kwa mujibu wa
ratiba ya Tume ya Uchaguzi kura za mchujo zinapasa kumalizika tarehe 27
Aprili.
Kuingia kwa Gavana wa Bomet Isaac Ruto katika Muungano
wa NASA kumeanza kuleta tumbojoto kwa chama kinachotawala cha Julilee
huku taswira ya siasa za Mwaka 2002 ikijitokeza wakati ambapo chama
tawala cha KANU kilibanduliwa mamlakani na muungano wa upinzani wa
National Rainbow Coalition NARC.
0 comments: