Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewaagiza madereva wa daladala na
bajaji kuhakikisha vyombo vyao vya usafiri vinakuwa na kikapu cha
kuwekea taka, vinginevyo watatozwa faini ya uchafuzi wa mazingira.
Akizungumza
leo jijini Dar es Salaam katika kufanya kwa vitendo kampeni ya usafi ya
kila jumamosi ya mwisho wa mwezi DC Mjema alitembelea kituo cha
daladala cha stesheni na kukuta magari mengi ya abiria hayana vikapo vya
taka, ambapo wameyatoza takribani magari saba kiasi cha shilingi 50000
kwa kila moja katika eneo hilo.
Huku
kwa upande wa madereva wa bajaji wanaopaki eneo la Soko la Samaki Feri
wamepewa onyo na kuombwa kufanya hivyo mara moja kabla hawajachuliwa
hatua na mamlaka husika ya Halmashauri hiyo ya Ilala.
Katika
hatua nyingine DC Mjema amewataka wafanyabishara wadogo wanaopanga
bidhaa zao kandokando ya barabara iliyopo jirani na soko la samaki Feri
kujiandikisha kwa afisa mtendaji na kuondoka eneo hilo mara moja, huku
Halmashauri hiyo itawapangia maeneo ya biashara ndani ya soko hilo la
samaki la Feri.
0 comments: