MEJA JENERALI JA'FARI : MAPINDIZI YA KIISLAMU YA IRAN YAMEFANIKIWA KUKABILIANA NA VITISHO

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu Iran (SEPAH) amesema kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yamepata mafanikio katika nyuga zote katika kukabiliana na vitisho vya kijeshi, kiusalama na kisiasa.
Meja Jenerali Mohammad Ali Jafari amesema hayo leo katika Kongamano la Malik Ashtar mjini Tehran na kubainisha kwamba, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yana izza, heshima na yako hai na kwamba, yanasonga mbele kuelekea katika malengo makuu.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu Iran (SEPAH) sambamba na kusisitiza kwamba, msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kuwatetea Waislamu na wanaodhulumiwa amesema kuwa, huko Lebanon, Syria na Yemen, Mapinduzi ya Kiislamu yanafuatilia kuyaunga mkono mataifa madhlumu na yanayokabiliwa na dhulma.
Meja Jenerali Muhammad Ali Ja'fari, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu Iran (SEPAH) 
Meja Jenerali Muhammad Ali Ja'fari amesema bayana kwamba, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH limo katika kukabiliana na vitisho na hatari zinazoyakabili mapinduzi haya na kwamba limekuwa na nafasi muhimu katika uwanja huo.
Aidha Kamanda Mkuu wa Jeshi la Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu Iran (SEPAH) amesema kuwa, hadi sasa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameweza kuvigeuza vitisho vyote na kuvifanya kuwa fursa na kwamba, moja ya matunda ya vita vya kulazimishwa vilivyoanzishwa na utawala wa dikteta wa wakati huo wa Iraq Saddam Hussein dhidi ya taifa hili ni kuenea fikra za Mapinduzi ya Kiislamu katika Mashariki ya Kati na ulimwenguni.

0 comments: